Tuesday, September 4, 2012

MAN UNITED KUMSAJILI LEANDRO DAMIAO ALIYETISHA NA BRAZIL OLIMPIKI YA LONDON


Hot property: Brazil striker Leandro Damiao has attracted several big clubs
Leandro Damiao anavutia klabu kadhaa kubwa Ulaya


Manchester United inataka kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Leandro Damiao katika dirisha dogo Januari.
Tottenham ilishindwa kumsajili kwa dau la pauni Milioni 20 Damiao wiki iliyopita, wakati nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 alipewa ofa ya kwenda kwa mkopo Liverpool, lakini dili hilo lilishindikana kwa sababu ya gharama. 
United inafanya mazungumzo juu ya Damiao na imekutana na wawakilishi wake Uwanja wa ndege wa Sao Paulo jana kuzungumzia uwezekano wa uhamisho wa Januari. 
United iliimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa usajili wa pauni Milioni 24 wa Robin van Persie kutoka Arsenal na sasa safu hiyo inatarajiwa kuwa tishio ikiwa na wakali wengine akina Danny Welbeck, Wayne Rooney na Javier Hernandez 'Chicharito'.
Lakini Leandro anakuja kwa kasi katika orodha ya wanasoka baab kubwa duniani, baada nyota yake kung'ara kwenye Michezo ya Olimpiki mjini London mwaka huu, akiiwezesha Brazil kutwaa Medali ya Fedha.

CHELSEA, MAN CITY AU PSG MOJAWAPO KUMNUNUA RONALDO KWA PAUNI MILIONI 100



KLABU zenye 'hela chafu', PSG, Manchester City na Chelsea zinajipanga kumtwaa Cristiano Ronaldo, baada ya mshambuliaji huyo kusema hana furaha Real Madrid.
Ronaldo aligoma kushangilia mabao yake Real Madrid Jumapili na akasema baada ya mechi hiyo ni sababu za kimchezo.
Cheer up! Cristiano Ronaldo (pictured arriving at training on Monday) has said he is 'unhappy' with the current situation at Real Madrid
Cristiano Ronaldo (pichani akiwasili mazoezini jana) 
Cheer up! Cristiano Ronaldo (pictured arriving at training on Monday) has said he is 'unhappy' with the current situation at Real Madrid
Ronaldo anaingia Bernabeu

Klabu hizo tajiri kiasi cha kutosha zinaweza kutoa pauni Milioni 100 kuvunja mkataba wake Real uliobakiza miaka mitatu na zinaweza kumpa mshahara kuanzia pauni Milioni 1 kwa mwezi.
Jose Mourinho pia hatarajiwi kubaki Real, kuna uwezekano akaondoka msimu ujao na anaweza akamtanguliza Ronaldo sehemu atakayokwenda, zaidi City na PSG zikipewa nafasi kubwa.
Mshambuliaji huyo Mreno, alisajiliwa kutoka Manchester United kwa pauni Milioni 80 mwaka 2009, na hadi sasa ameipa Real taji la La Liga msimu uliopita, akifunga mabao 46 katika mechi 38  na mabao 60 katika mashindano yote, kiwango ambacho mchezaji huyo mwenhye umri wa miaka 27 anafikiri hakiendani na maslahi duni anayopata hapo.
Amefunga mabao 150 katika klabu hiyo, kiwango ambacho ni zaidi ya bao moja katika kila mechi, lakini bado anafunikwa Lionel Messi wa Barcelona. Wengine wanasema Messi ndiye anayemnyima raha kiasi cha kufikiria kuondoka.
Ouch! Ronaldo was substituted in Sunday's 3-0 win over Granada at the Bernabeu
Ronaldo alitolewa Jumapili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Granada Uwanja wa Bernabeu baada ya kuumia
Is that it? Ronaldo failed to show much enthusiasm as he bagged two goals in the game
Aliwapungia tu mikono mashabiki baada ya kufunga juzi

Wakati alipoboronga akiichezea timu yake ya taifa, Ureno dhidi ya Denmark katika Euro 2012, mashabiki wa Denmark walimzomea wakitaja jina la Messi.
Ronaldo hapewi hadhi kubwa Real kama Messi anayopewa Barca na kituo kimoja cha Redio kiliripoti kwamba alikuwa na mazungumzo na raia wa klabu, Florentino Perez akilalamikia kutopewa sapoti katika chumba cha kubadilishia nguo.
Lakini pia na kukosa tuzo ya Mwanasoka Bora Ulaya mbele ya Andres Iniesta wiki iliyopita, kunaongeza machungu kwenye moyo wake.
Unhappy chappy: Ronaldo said he was 'sad' but refused to elaborate on the reasons why
Ronaldo akiwa benchi baada ya kutoka Jumapili
Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2197885/Cristiano-Ronaldo-alerts-Man-City-Chelsea-PSG.html#ixzz25THGHhii

Vituko 5 vya usajili Bara kihistoria, mtu mzima Rage kumwaga chozi kali zaidi


Mbuyu Tweite aka Rage

USAJILI wa Ligi Kuu ya Bara msimu huu umekuwa na msisimko wa aina yake, kutokana na ‘umafia’ waliofanyiana watani wa jadi, Simba na Yanga- jambo ambalo limekumbushia baadhi ya matukio ya aina hiyo miaka iliyopita, kama lile la Victor Costa kusaini Yanga na kujiunga nao, kisha kurejea Simba na kuvaa jezi yenye jina la aliyempa fedha kusaini fomu Jangwani, Jamal Malinzi, aliyekuwa Katibu wa Yanga wakati huo. Safari hii, Mbuyu Twite alipewa dola za Kimarekani 30,000 na Ismail Aden Rage, Mwenyekiti wa Simba na kusaini, lakini akasaini pia na kuhamia Yanga kutoka APR na alipofika Dar es Salaam akavaa jezi yenye jina la Mtanzania huyo mwenye asili ya Kisomali. DIMBANI LEOinakukumbusha baadhi ya vituko hivyo na kuamua kukipa ‘namba moja’ kituo cha Rage.
YUSSUF ISMAIL BANA
Yussuf Bana kushoto akiichezea Yanga dhiai ya Simba. Kulia ni Zamoyoni Mogella na nyuma ni Muhiddin Cheupe.
AKIWA mchezaji wa Pamba ya Mwanza mwanzoni mwa miaka ya 1980, beki Yussuf Ismail Bana alisaini Simba katika fomu za usajili akitumia jina la Yussuf Ismail. Lakini baadaye Yanga wakamfuata na kumrubuni asaini kwao. Akasaini Jangwani na kutumia jina la Yussuf Bana na Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa TFF) chini ya Mwenyekiti wake wa enzi hizo, Said Hamad El Maamry wakamuidhinisha kuchezea Yanga, lilikuwa bonge la sinema.
CHARLES BONIFACE MKWASA
Charles Boniface Mkwasa
Akiwa mchezaji mpya kwenye kikosi cha Yanga aliyesajiliwa kutoka Tumbaku ya Morogoro, mwanzoni mwa miaka ya 1980, Simba ilimfuata na kumrubuni ahamie kwao. Kiungo Charles Boniface Mkwasa, akakubali na kusaini Simba SC kwa jina la Charles Boniface alilokuwa pia akitumia Yanga na tangu Tumbaku. Lakini Yanga wakamfuata na kumshawishi abaki, na baada ya kukubaliana naye, akasaini kuendelea kuichezea Yanga, safari hii akitumia jina la Charles Boniface Mkwasa. Lakini hii mbele ya FAT ya El Maamry ilidunda na Mkwasa alifungiwa msimu mzima kabla ya kumaliza adhabu yake na kuendelea kucheza Jangwani. 
EPHRAIM MAKOYE MAHALA:
Akiwa mchezaji mpya kwenye kikosi cha Yanga aliyesajiliwa kutoka Kagera Stars mwaka 2000 (sasa Kagera Sugar), Simba SC walimfuata na kumrubuni asaini kwao. Makoye, ambaye wakati huo alikuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika sekondari ya Makongo, alichukua fedha za Simba akasiani. Hata hivyo, siku hiyo hiyo Yanga walimnasa na kumchukua hadi kwa viongozi wa Simba kurudisha fedha alizochukua aendelee kuchezea Yanga. Simba waligoma kuchukua fedha na kwa sababu wakati huo FAT ilikuwa haitambui mikataba ya klabu na mchezaji zaidi ya fomu za usajili, ambazo zilikuwa hazijatoka, Makoye aliendelea kuchezea Yanga, ingawa baadaye alichezea Simba alipotemwa Yanga. 
VICTOR COSTA
Victor Costa aka Malinzi
Akiwa mchezaji mpya aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar kwenye kikosi cha Simba mwaka 2005, Yanga walimfuata beki huyo na kumrubuni asaini kwao. Costa alisaini na kwenda kujiunga na wenzake kambini Zanzibar ambako timu ilikuwa inacheza Kombe la Mapinduzi. Lakini aliporejea tu Dar es Salaam, Simba wakamteka na kumpeleka mazoezini kwao, akiwa amevaa jezi iliyoandikwa jina la Katibu Mkuu wa Yanga wakati huo, Jamal Malinzi. Costa hakurudisha fedha za Yanga na akaidhinishwa kuendelea kuchezea timu yake. 
MBUYU TWITE:
Akiwa amekwishasaini mkataba wa kuichezea Simba SC kutoka APR ya Rwanda, Yanga wakamzungukia na kumsainisha na beki huyo akaamua kurudisha fedha za Simba. Tukio hilo lilimtoa machozi Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dodoma kulaani kitendo hicho. Tukio hilo siyo tu linapanda kileleni katika vituko vya usajili wa Ligi Kuu ya Bara kwa sababu ndilo la sasa, bali pia kwa kitendo cha ‘mtu mzima’ Rage kumwaga machozi mbele ya kamera za Televisheni akisikitikia changa la macho alilopigwa na mchezaji huyo.  
Rage akilia huku akiwa amekumbatiwa vizuri na kubembelezwa na Profesa Philemon Sarungi. Hapa ilikuwa kwenye msiba wa Patrick Mafisango.
HITIMISHO: Yapo matukio mengine ya wachezaji kuchukua fedha timu nyingine na kubaki timu zao kama Amri Said mwaka 2002, lakini hayana msisimko kwa sababu hawakuwahi kujiunga na timu mpya- haya matano ndio yalikwishatengeneza picha fulani, kwamba mchezaji fulani sasa ni wa timu fulani, lakini baadaye akageuza kibao

ARSENAL YATAMKA WAZI; MAN CITY, MAN UNITED, CHELSEA HATUWAWEZI



Mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood amesema klabu yake haiwezi kushindana sokoni na wapinzani wao wakubwa katika Top Four ya Ligi Kuu ya England kwa sababu wanatumia fedha nyingi.
Lakini Hill-Wood anajiamini The Gunners watashinda taji moja muhimu msimu huu na amesema hawana wasiwasi wowote kwa Arsene Wenger kutoshinda taji lolote ndani ya miaka saba.
Mwenyekiti huyo wa Arsenal, alisema; "Arsene ana fedha za kutumia, lakini zina kiwango. Hatuwezi kutumia pauni Milioni 50 kwa mchezaji mmoja,"alisema.
Off and running: Arsenal beat Liverpool to earn their first three points
Arsenal iliifunga Liverpool mwishoni mwa wiki na kuingiza pointi tatu za kwanza

MATAMSHI YA RAGE YAVURUGA KIKAO CHA SULUHU SIMBA NA YANGA KUHUSU TWITE, YONDAN

Mbuyu Twite


KLABU za Simba na Yanga zimeshindwa kufikia suluhu mbele ya Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa, katika kikao cha leo, juu ya wachezaji Kevin Yondan na Mbuyu Twite.
Katika kikao hicho kilichoanza majira ya saa 7:00 mchana, hoja ya kwanza kuwasilishwa mezani ilikuwa ni suala la beki Twite na upande wa Yanga uliwakilishwa na Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Katibu, Celestine Mwesigwa wakati kwa Simba walikuwepo Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe.
Ikumbukwe, Simba iliwasilisha malalamiko ya kufanyiwa mchezo usio wa kiungwana na Yanga kwa Twite. Ilidai Twite alisaini mkataba na klabu yao Agosti 1, mwaka huu mbele yao, viongozi wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na APR na kulipwa dola za Kimarekani 30,000 na nyingine 2,000 za nauli ya kuja Dar es Salaam kujiunga na klabu hiyo. Hata hivyo, mchezaji huyo akahamia Yanga.
Katika mjadala huo, Simba ilikubali kurudishiwa fedha zao, lakini viongozi wa Yanga wakasema hawawezi kutoa hadi waombwe radhi na Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, ambaye alisema viongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani wana ‘fedha chafu za EPA’.
Simba wakasema kauli yake ya Rage ilikuwa sehemu ya utani wa jadi, kama ambavyo Yanga walimvalisha jezi Twite yenye jina la Rage.
Kufikia hapo, Simba wakasema hawawezi hata kujadili suala la Kevin Yondan na Kamati ya Mgongolwa ikasema itapitia maelezo ya pande zote, watatoa majibu kwa mujibu wa kanuni na sheria Septemba 10, mwaka huu.
Katika kesi ya Yondan, walalamikaji ni Simba, ambao wanadai beki huyo alisaini Yanga akiwa bado ana mkataba na klabu yao.
Awali, Kamati ya Mgongolwa ilikutana Jumapili asubuhi hadi usiku, bila kupata suluhisho la pingamizi hizo na kuamua kutumia busara ya kuzikutanisha pande zinazopingana kujaribu kupata suluhu leo.
Pingamizi nyingine zilikuwa ni, Azam inayopinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani na inaelezwa tayari klabu hizo zimekwishamalizana juu ya kiungo huyo.
Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo kwa maelezo walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/2013.
Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa kwa maelezo inao wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano. Imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.
Pingamizi nyingine ambazo jumla zinahusu wachezaji 17 walioombewa usajili katika timu za Ligi Kuu ni Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlington aliyeombewa usajili Kagera Sugar, na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao.
Pia Flamingo ya Arusha inapinga usajili wa wachezaji wake Kelvin Friday Iddy katika timu za Azam na Salim Walii (Polisi Mara) kwa vile taratibu za kuwahamisha bado hazijafanywa. Nayo Kagera Sugar inapinga usajili wa beki David Charles Luhende kwenda Yanga kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa.
Super Falcon ya Chanjamjawiri, Chakechake, Pemba inapinga wachezaji wake wanne; Edward Christopher Shija, Samir Said Luhava (Simba), Robert Joseph Mkhotya (African Lyon) na Sultan Juma Shija (Coastal Union) kusajiliwa katika timu hizo kwa maelezo taratibu halali za uhamisho hazikufuatwa.
Mchezaji Othman Hassan aliyeombewa usajili Coastal Union anapingwa na Oljoro JKT kwa vile bado ana mkataba na timu hiyo unaomalizika Mei 24, 2013. Nayo Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy kutoka Yanga kwenda Simba hadi itakapolipwa fidia ya kumlea mchezaji huyo kwa vile bado hajafikisha umri wa miaka 23

Zenit yawasajili Hulk, Witsel


Jumanne, 04 Septemba 2012 09:16

HULKKlabu Bingwa ya Urusi, Zenit St Petersburg, imetangaza kuwanasa kwa mpigo Straika wa Brazil Hulk kutoka FC Porto na Kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel kutoka Benfica.
Wachezaji hao wawili tayari wameshaini Mikataba ya Miaka mitano kila mmoja.
Dili hizi za kuwanasa Wachezaji hao zilitangazwa rasmi kwenye Tovuti ya Klabu hiyo na iliwapa hongera Mashabiki wake kwa habari hizo nzuri.
Hata hivyo, hadi sasa haikutajwa Wachezaji hao wamenunuliwa kwa Dau lipi lakini inasemekana Wakala wa Hulk, Teodoro Fonseca, alitamka kuwa Hulk amenunuliwa kwa Euro Milioni 60.
Hulk, mwenye Miaka 26 ambae alijiunga na FC Porto akitokea Ligi ya Japan Mwaka 2008, ameshatwaa Ubingwa wa Ureno mara 3 pamoja na Taji la Europa Ligi Mwaka 2011 na ameifungia Brazil goli 5 katika Mechi 14 alizocheza.
Nae Witsel, Miaka 23, inadaiwa amesajiliwa na Zenit kwa Dau la Euro Milioni 40 na alijiunga na Benfica Julai 2011 akitokea Standard Liege ambayo ilimuuza kwa Ada ya Euro Milioni 8.

Serengeti Boys kupiga Kambi Mbeya!


Jumanne, 04 Septemba 2012 16:34
Chapisha Toleo la kuchapisha
TFF_LOGO>>KUCHEZA na Mbeya City na Prisons
LEO TFF, Shirikisho la Soka Tanzania, limetoa Taarifa iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Sunday Kayuni, kwamba Timu ya Taifa ya Vijana wa umri wa chini ya Miaka 17, Serengeti Boys, wamesafiri leo kwenda Mkoani Mbeya ili kupiga Kambi ya maandalizi kwa ajili kupambana na wenzao wa Misri kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Vijana Barani Afrika huko Nchini Morocco Mwaka 2013.
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI YA TFF:
04 Septemba, 2012.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Timu yetu ya taifa ya vijana wa umri wa chini ya miaka kumi na saba (U.17) Serengeti Boys, wameondoka leo asubuhi kwenda mkoani Mbeya kuendelea na maandalizi ya kufuzu fainali za vijana zitazofanyika nchini Morocco mwaka 2013. Timu yetu imepangiwa kupambana na timu ya taifa ya vijana wa Misri (Egypt) katika hatua inayofuata, pambano hilo linatarajia kufanyika Oktoba 2012. Timu yetu ilipata ushindi baada ya timu ya vijana ya Kenya kujitoa kwenye michuano hii.
Timu imekwenda mkoani Mbeya kwa mwaliko wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya ya Mbeya Mjini (MUFA), ikiwa huko chama hicho kitaihudumia kwa malazi, chakula na huduma nyingine ndogondogo. Timu inategemea kupangiwa michezo kadhaa ya majaribio na timu kabambe za mkoani humo ikiwemo Mbeya City, Tanzania Prisons na timu za kombaini.
Shirikisho la  Mpira wa Miguu nchini linapenda kutumia fursa hii kuishukuru na kuipongeza MUFA, kwa kuonyesha mfano unaostahili kuigwa na wadau wengine, wa kushirikiana katika maandalizi ya kuziandaa timu zetu za taifa. Kitendo hicho kinaonyesha kuguswa, uwajibikaji, uzalendo na ukomavu katika kutatua matatizo kwa vitendo na sio kwa lawama bila suluhisho.
Shirikisho pia linaishukuru benki ya NMB kwa kutoa msaada wa jezi seti moja na fedha sh. Millioni tano, zilizowezesha vijana hawa kupata posho zao za kambi na kusafiri kwenda Mbeya. Itakumbukwa kuwa benki ya NMB imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya soka ya vijana kwa muda mrefu sasa. Kwa kipindi cha miaka sita (2006-2010) iliyopita ilidhamini mafunzo ya makocha wanaojihusisha na program za maendeleo ya vijana nchini, vilevile ilitoa mipira ya program za vijana kwa vyama vya mikoa. Hivyo tunaishukuru kwa kuthamini mchango wao huo na kwa kuendelea kutoa msaada ili kuhahakisha inalinda mafanikio ya program hizo.
Shirikisho linapenda kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia kuwaandaa vijana wetu hawa pekee waliobaki kwenye mashindano. Mafanikio ya timu yetu ya taifa (Taifa Stars) siku za usoni yanategemea sana msingi bora wa vijana hawa. Hivyo ni vema tukashirikiana kama walivyojitokeza MUFA na NMB.
Hutisiti kueleza bayana kuwa kama si wadau hawa kambi ya vijana ilikuwa inavunjika, na baada ya kurudi Mbeya kama hakutakuwa na wadau wengine watakaojitokeza basi uwezo wa kuendelea na kambi ya maandalizi kwa vijana wetu utakuwa finyu mno.
Shirikisho lina imani kuwa wakazi wa Mbeya watatoa ushirikiano wa hali ya juu wakiongozwa na Chama cha Mpira cha Mkoa (MREFA), kwa Serengeti Boys ili kufanikisha maandalizi hayo.
Sunday Kayuni
Kaimu  Katibu Mkuu

KOMBE la DUNIA 2014: Ulaya kurindima kuanzia Ijumaa!


Jumanne, 04 Septemba 2012 18:57

BRAZIL_2014_ORIJINO11>>KWINGINEKO nako wamo, Afrika Mwakani!
>>ULAYA hamna Mechi za Ligi za Klabu Wikiendi hii!!
Ukitoa Bara la Afrika ambao hawatacheza Mechi zao Wiki hii kwa vile walishaanza mchakato wao wa kupata wawakilishi wao wa kwenda Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil huku Mechi zao kuendelea Machi Mwakani, Barani Ulaya Ijumaa hii ndio wataingia dimbani kwa mara ya kwanza na huko Marekani ya Kusini, Asia na kwingineko watakuwa wakiendelea na Mechi zao.
Huko Ulaya, Makundi yote 9 yatakuwa kilingeni Ijumaa na Jumamosi kwa Mechi zao za kwanza na zile za pili kuchezwa Jumanne ijayo.
Hali kadhalika kwa Marekani ya Kusini ambao nao watacheza Siku kama hizo.
Mechi hizi za Timu za Taifa zinafanya Ligi za Barani Ulaya kupumzika hadi Wikiendi itakayoanzia Septemba 14.
Zifuatazo ni Ratiba ya Mechi za huko Marekani ya Kusini na Ulaya:
KANDA ya MAREKANI ya KUSINI
RATIBA
[Saa ni za Bongo]
Ijumaa Septemba 7
23:30 Colombia v Uruguay
Jumamosi September 8
0:00 Ecuado v Bolivia
2:10 Argentina v Paraguay
4:25 Peru v Venezuela
Jumanne Septemba 11
22:30 Chile v Colombia
Jumatano Septemba 12
0:30 Uruguay v Ecuador
2:25 Paraguay v Venezuela
4:25 Peru v Argentina
MSIMAMO:
1 Chile Mechi 6 Pointi 12
2 Uruguay Mechi 5 Pointi 11
3 Argentina Mechi 5 Pointi 10
4 Ecuador Mechi 5 Pointi 9
5 Venezuela Mechi 6 Pointi 8
5 Colombia Mechi 5 Pointi 7
7 Bolivia Mechi 6 Pointi 4
8 Paraguay Mechi 5 Pointi 4
8 Peru Mechi 5 Pointi 3
FAHAMU: Timu 4 za juu zinatinga Fainali Brazil moja kwa moja na ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo.
KANDA ya ULAYA
RATIBA
[Saa ni za Bongo]
Ijumaa Septemba 7
19:00 Azerbaijan v Israel [Kundi F]
19:00 Russia v  Northern Ireland [Kundi F]
19:00 Kazakstan v Ireland [Kundi C]
20:00 Liechtenstein v Bosnia And Herzegovina [Kundi G]
20:00 Georgia v Belarus [Kundi I]
21:00 Malta v Armenia [Kundi B]
21:00 Estonia v Romania [Kundi D]
21:15 Croatia v Macedonia [Kundi A]
21:30 Slovenia v Switzerland [Kundi E]
21:30 Netherlands vTurkey [Kundi D]
21:30 Latvia v Greece [Kundi G]
21:30 Andorra v Hungary [Kundi D]
21:30 Finland v France [Kundi I]
21:30 Montenegro v Poland [Kundi H]
21:45 Luxembourg v Portugal [Kundi F]
21:45 Moldova v England [Kundi H]
21:45 Germany v Faroe Islands [Kundi C]
21:45 Iceland v Norway [Kundi E]
21:45 Bulgaria v Italy [Kundi B]
21:45 Wales v Belgium [Kundi A]
22:15 Lithuania v Slovakia [Kundi G]
22:30 Albania v Cyprus [Kundi E]
Jumamosi September 8
17:00 Scotland v Serbia [Kundi A]
21:15 Denmark v Czech Republic [Kundi B]
Jumanne Septemba 11
20:00 Israel v Russia [Kundi F]
20:00 Cyprus v Iceland [Kundi E]
20:30 Romania v Andorra [Kundi D]
20:30 Georgia v Spain [Kundi I]
21:00 Norway v Slovenia [Kundi E]
21:00 Turkey v Estonia [Kundi D]
21:00 Bulgaria v Armenia [Kundi B]
21:15 Bosnia And Herzegovina v Latvia [Kundi G]
21:15 Slovakia v Liechtenstein [Kundi G]
21:30 Austria v Germany [Kundi C]
21:30 Sweden v Kazakstan [Kundi C]
21:30 Hungary v Netherlands [Kundi D]
21:30 San Marino v Montenegro [Kundi H]
21:30 Switzerland v Albania [Kundi E]
21:30 Serbia v Wales [Kundi A]
21:45 Poland v Moldova [Kundi H]
21:45 Northern Ireland v Luxembourg [Kundi F]
21:45 Greece v Lithuania [Kundi G]
21:45 Belgium v Croatia [Kundi A]
21:45 Italy v Malta [Kundi B]
22:00 France v Belarus [Kundi I]
22:00 Scotland v Macedonia [Kundi A]
22:00 England v Ukraine [Kundi H]
23:00 Portugal v Azerbaijan [Kundi F]
MAKUNDI:
Kundi A
Belgium
Croatia
Macedonia
Scotland
Serbia
Wales
Kundi B
Armenia
Bulgaria
Czech Republic
Denmark
Italy
Malta
Kundi C
Austria
Faroe Islands
Germany
Kazakhstan
Republic of Ireland
Sweden
Kundi D
Andorra
Estonia
Hungary
Netherlands
Romania
Turkey
Kundi E
Albania
Cyprus
Iceland
Norway
Slovenia
Switzerland
Kundi F
Azerbaijan
Israel
Luxembourg
Northern Ireland
Portugal
Russia
Kundi G
Bosnia and Herzegovina
Greece
Latvia
Liechtenstein
Lithuania
Slovakia
Kundi H
England
Moldova
Montenegro
Poland
San Marino
Ukraine
Kundi I
Belarus
Finland
France
Georgia
Spain
FAHAMU: Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.

Nyekundu Huddlestone yafutwa, Owen atua Stoke, Malouda nje Chelsea ya Ulaya!


Jumanne, 04 Septemba 2012 20:11
Chapisha Toleo la kuchapisha
michael_owen3>>DIARRA huyooo MAKHACHKALA!!
Zifuatazo ni habari fupi fupi za Soka  ambazo zinahusu Kiungo wa Tottenham, Tom Huddlestone, kufutiwa Kadi Nyekundu, Straika wa zamani wa Manchester United Michael Owen kujiunga na Stoke, Chelsea kumuacha Florent Malouda kwenye Kikosi chake cha Ulaya na Kiungo wa Real Madrid Lassana Diarra kuhamia to Anzhi Makhachkala.
Tom Huddlestone afutiwa Nyekundu!
Kiungo wa Tottenham Hotspur Tom Huddlestone amefutiwa Kadi Nyekundu aliyopewa kwenye Mechi ya Ligi Kuu England walipotoka sare 1-1 na Norwich City Uwanja wa White Hart Lane Jumamosi iliyopita.
Huddlestone, ambae aliingizwa toka Benchi Kipindi cha Pili ili kucheza Mechi yake ya kwanza kwa zaidi ya Mwaka baada ya kuwa majeruhi, alipewa Kadi Nyekundu na Refa Mark Halsey katika Dakika ya 90 kwa rafu kwa Jonny Howson, rafu ambayo marudio yake kwenye TV yalionyesha haikustahili Kadi yeyote.
Tottenham walikata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu na wameshinda hivyo Mchezaji huyo yuko huru kucheza Mechi yao inayofuata hapo Septemba 16 ugenini na Reading.
Michael Owen
Zipo taarifa thabiti kuwa Michael Owen ametua Stoke City ili kukamilisha usajili wake kwa Mkataba wa Miaka miwili ambao unaaminika utakuwa na kipengele cha yeye kulipwa tu ikiwa atacheza Mechi kutokana na historia yake ya kuumia mara kwa mara.
Owen, Miaka 32, yuko huru kujiunga na Klabu yeyote hivi sasa kwa vile Klabu yake Manchester United imemuacha hivyo hazuiwi kujiunga na Klabu nyingine licha ya Dirisha la Uhamisho kufungwa Agosti 31.
Malouda atemwa Ulaya!
Chelsea imemuacha Florent Malouda katika Kikosi chao cha Wachezaji 22 ambao wamesajiliwa UEFA kucheza hatua ya Makundi ya CHAMPIONZ LIGI.
Tangu Msimu huu uanze, Malouda, Miaka 32, amekuwa hayumo kwenye Kikosi chochote cha Mabingwa wa Ulaya Chelsea ambacho kimekuwa kikicheza Mechi za Ligi Kuu England.
Hivi karibuni Chelsea imekuwa ikiwatoa Wachezaji wake ambao ni pamoja na Raul Meireles aliejiunga na Fenerbahce Jumatatu na Michael Essien aliehamia kwa mkopo Real Madrid Ijumaa iliyopita.
Pamoja na Malouda, Kipa veterani Hilario nae hayumo kwenye Kikosi hicho cha UEFA.
Diarra yupo Urusi!
Kiungo wa Real Madrid Lassana Diarra amekamilisha Uhamisho wake kwa Mabingwa wa Urusi Anzhi Makhachkala kwa kusaini Mkataba wa Miaka minne.
Mapema juzi Real Madrid ilitangaza Diarra atahamia Anzhi Makhachkala mkopo wa Msimu mmoja lakini sasa hilo limebadilika baada ya yeye kusaini Mkataba wa kudumu.
Huko Anzhi Makhachkala, Diarra anaungana na Majina maarufu wakiwemo Samuel Eto'o, Christopher Samba na Yuri Zhirkov.
Diarra alijiunga na Real Madrid Januari Mwaka 2009 akitokea Portsmouth.