Tuesday, September 4, 2012

ARSENAL YATAMKA WAZI; MAN CITY, MAN UNITED, CHELSEA HATUWAWEZI



Mwenyekiti wa Arsenal, Peter Hill-Wood amesema klabu yake haiwezi kushindana sokoni na wapinzani wao wakubwa katika Top Four ya Ligi Kuu ya England kwa sababu wanatumia fedha nyingi.
Lakini Hill-Wood anajiamini The Gunners watashinda taji moja muhimu msimu huu na amesema hawana wasiwasi wowote kwa Arsene Wenger kutoshinda taji lolote ndani ya miaka saba.
Mwenyekiti huyo wa Arsenal, alisema; "Arsene ana fedha za kutumia, lakini zina kiwango. Hatuwezi kutumia pauni Milioni 50 kwa mchezaji mmoja,"alisema.
Off and running: Arsenal beat Liverpool to earn their first three points
Arsenal iliifunga Liverpool mwishoni mwa wiki na kuingiza pointi tatu za kwanza

No comments:

Post a Comment