KLABU zenye 'hela chafu', PSG, Manchester City na Chelsea zinajipanga kumtwaa Cristiano Ronaldo, baada ya mshambuliaji huyo kusema hana furaha Real Madrid.
Ronaldo aligoma kushangilia mabao yake Real Madrid Jumapili na akasema baada ya mechi hiyo ni sababu za kimchezo.

Cristiano Ronaldo (pichani akiwasili mazoezini jana)
![]() |
Ronaldo anaingia Bernabeu |
Klabu hizo tajiri kiasi cha kutosha zinaweza kutoa pauni Milioni 100 kuvunja mkataba wake Real uliobakiza miaka mitatu na zinaweza kumpa mshahara kuanzia pauni Milioni 1 kwa mwezi.
Jose Mourinho pia hatarajiwi kubaki Real, kuna uwezekano akaondoka msimu ujao na anaweza akamtanguliza Ronaldo sehemu atakayokwenda, zaidi City na PSG zikipewa nafasi kubwa.
Mshambuliaji huyo Mreno, alisajiliwa kutoka Manchester United kwa pauni Milioni 80 mwaka 2009, na hadi sasa ameipa Real taji la La Liga msimu uliopita, akifunga mabao 46 katika mechi 38 na mabao 60 katika mashindano yote, kiwango ambacho mchezaji huyo mwenhye umri wa miaka 27 anafikiri hakiendani na maslahi duni anayopata hapo.
Amefunga mabao 150 katika klabu hiyo, kiwango ambacho ni zaidi ya bao moja katika kila mechi, lakini bado anafunikwa Lionel Messi wa Barcelona. Wengine wanasema Messi ndiye anayemnyima raha kiasi cha kufikiria kuondoka.

Ronaldo alitolewa Jumapili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Granada Uwanja wa Bernabeu baada ya kuumia

Aliwapungia tu mikono mashabiki baada ya kufunga juzi
Wakati alipoboronga akiichezea timu yake ya taifa, Ureno dhidi ya Denmark katika Euro 2012, mashabiki wa Denmark walimzomea wakitaja jina la Messi.
Ronaldo hapewi hadhi kubwa Real kama Messi anayopewa Barca na kituo kimoja cha Redio kiliripoti kwamba alikuwa na mazungumzo na raia wa klabu, Florentino Perez akilalamikia kutopewa sapoti katika chumba cha kubadilishia nguo.
Lakini pia na kukosa tuzo ya Mwanasoka Bora Ulaya mbele ya Andres Iniesta wiki iliyopita, kunaongeza machungu kwenye moyo wake.

Ronaldo akiwa benchi baada ya kutoka Jumapili
No comments:
Post a Comment