
Leandro Damiao anavutia klabu kadhaa kubwa Ulaya
Manchester United inataka kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Leandro Damiao katika dirisha dogo Januari.
Tottenham ilishindwa kumsajili kwa dau la pauni Milioni 20 Damiao wiki iliyopita, wakati nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 alipewa ofa ya kwenda kwa mkopo Liverpool, lakini dili hilo lilishindikana kwa sababu ya gharama.
United inafanya mazungumzo juu ya Damiao na imekutana na wawakilishi wake Uwanja wa ndege wa Sao Paulo jana kuzungumzia uwezekano wa uhamisho wa Januari.
United iliimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa usajili wa pauni Milioni 24 wa Robin van Persie kutoka Arsenal na sasa safu hiyo inatarajiwa kuwa tishio ikiwa na wakali wengine akina Danny Welbeck, Wayne Rooney na Javier Hernandez 'Chicharito'.
Lakini Leandro anakuja kwa kasi katika orodha ya wanasoka baab kubwa duniani, baada nyota yake kung'ara kwenye Michezo ya Olimpiki mjini London mwaka huu, akiiwezesha Brazil kutwaa Medali ya Fedha.
No comments:
Post a Comment