Tuesday, September 4, 2012

Zenit yawasajili Hulk, Witsel


Jumanne, 04 Septemba 2012 09:16

HULKKlabu Bingwa ya Urusi, Zenit St Petersburg, imetangaza kuwanasa kwa mpigo Straika wa Brazil Hulk kutoka FC Porto na Kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel kutoka Benfica.
Wachezaji hao wawili tayari wameshaini Mikataba ya Miaka mitano kila mmoja.
Dili hizi za kuwanasa Wachezaji hao zilitangazwa rasmi kwenye Tovuti ya Klabu hiyo na iliwapa hongera Mashabiki wake kwa habari hizo nzuri.
Hata hivyo, hadi sasa haikutajwa Wachezaji hao wamenunuliwa kwa Dau lipi lakini inasemekana Wakala wa Hulk, Teodoro Fonseca, alitamka kuwa Hulk amenunuliwa kwa Euro Milioni 60.
Hulk, mwenye Miaka 26 ambae alijiunga na FC Porto akitokea Ligi ya Japan Mwaka 2008, ameshatwaa Ubingwa wa Ureno mara 3 pamoja na Taji la Europa Ligi Mwaka 2011 na ameifungia Brazil goli 5 katika Mechi 14 alizocheza.
Nae Witsel, Miaka 23, inadaiwa amesajiliwa na Zenit kwa Dau la Euro Milioni 40 na alijiunga na Benfica Julai 2011 akitokea Standard Liege ambayo ilimuuza kwa Ada ya Euro Milioni 8.

No comments:

Post a Comment