Alhamisi, 01 Novemba 2012 15:50
>>DESEMBA 19, Gremio Arena, Porto Alegre, Brazil.
Magwiji, ambao pia ni Mabalozi maalum wa
UNDP, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Ronaldo na Zidane,
wamealika Marafiki zao ili kucheza Mechi maalum ya Programu ya ‘Kupiga
vita Umasikini’ hapo Desemba 19 itakayochezwa Gremio Arena huko Porto
Alegre, Brazil.
Katika Mechi hii ya 10 ya ‘Kupiga vita
Umasikini’, Zidane na Ronaldo, ambao waliwahi kucheza pamoja Real
Madrid, kila mmoja atateua Kikosi chake.
Mechi za aina zimekuwa zikichezwa kila
Mwaka kuanzia Mwaka 2003, na kubarikiwa na FIFA pamoja na UEFA,
huchangisha Fedha ili kusaidia vita ya kuondoa Umaskini.
Kawaida Mechi hizi huchezwa katika Miji
tofauti kwa kuikutanisha Timu ya Mabalozi wa UNDP dhidi ya Timu ya Mji
inapochezwa lakini safari hii huko Gremio Arena, Porto Alegre, Brazil
zitakuwa ni Timu ya Ronaldo, ambae pia atashirikisha wenzake wa Brazil,
dhidi ya Timu ya Zidane.
Mwaka jana 2011, Mechi kama hii
ilichezwa Mjini Hamburg, Ujerumani kati ya Hamburger HSV na Timu ya UNDP
ambayo walikuwemo Ronaldo na Zidane.
Wachezaji wengine waliokuwemo kwenye
Mechi hiyo ni Didier Drogba (Ivory Coast), Dida (Brazil), Serginho
(Brazil), Jens Lehmann (Germany), Lucas Radebe (South Africa), Fernando
Hierro (Spain), Michel Salgado (Spain), Gheorghe Popescu (Romania),
Gheorghe Hagi (Romania), Luís Figo (Portugal), Fernando Couto
(Portugal), Christian Karembeu (France), Steve McManaman (England),
Pavel Nedved (Czech Republic), Fabio Cannavaro (Italy), na Sami Al-Jaber
(Saudi Arabia).
Mapato kwenye Mechi hizi huenda katika
Programu za kupiga vita Umasikini katika Nchi zaidi ya 27 za Marekani ya
Kusini, Africa na Asia.
Mapato makubwa ya Mechi ya Mwaka jana ya
huko Hamburg yalienda kusaidia balaa la njaa lililoikumba Kaskazini
Mashariki ya Afrika, hasa Somalia.
Akiongea Zidane alitamka: “Kila tunapokutana kwa Mechi hizi tunaweza kusaidia na kuleta tofauti kwa wenye shida!”
Nae Ronaldo amesema: “Ni muhimu kuonyesha umoja ili kusaidia wale wenye janga la Umasikini!”



No comments:
Post a Comment