Alhamisi, 01 Novemba 2012 21:26
>>BUNDESLIGA: Baada kichapo, vinara Bayern wataka faraja!
>>LA LIGA: Barca na Atletico zafukuzana, Real yajivuta!!
ZIFUATAZO ni Taarifa fupi kuhusu Ratiba na hali ya Ligi za Serie A, Bundesliga na La Liga:
SERIE A: Juve yawania kutofungwa Mechi ya 50 ikicheza na Inter Jumamosi!
RATIBA:
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
[SAA za BONGO]
Alhamisi Novemba 1
Genoa v Fiorentina [Comunale Luigi Ferraris]
Jumamosi Novemba 3
2000 AC Milan v Chievo Verona [Stadio Giuseppe Meazza]
2245 Juventus v Inter Milan [Juventus Stadium]
Jumapili Novemba 4
US Pescara v Parma [Adriatico]
Bologna v Udinese [Stadio Renato Della`Ara]
Catania v Lazio [Stadio Angelo Massimino]
Fiorentina v Cagliari [Stadio Artemio Franchi]
Napoli v Torino [Stadio San Paolo]
Sampdoria v Atalanta [Comunale Luigi Ferraris]
Siena v Genoa [Artemio Franchi]
AS Roma v Palermo [Stadio Olimpico]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Juventus wanaweza kuendeleza rekodi yao
ya kutofungwa katika Mechi 50 za Ligi ya Serie A Jumamosi watakapocheza
na Inter Milan ambao wako nafasi ya pili nyuma ya Juventus kwa Pointi 4.
Baada ya Mechi 10, Juventus wana Pointi
28 kwa kushinda Mechi zote kasoro sare katika Mechi moja tu lakini Inter
Milan wanakuja na moto baada ya kushinda Mechi zao 9 zilizopita, za
Ligi na Mashindano mengine, na hilo linaifanya Mechi hiyo kuwa ni tamu.
Juventus, ambao ndio Mabingwa watetezi,
walitwaa Taji Msimu uliopita bila kufungwa hata Mechi moja na mara ya
mwisho kufungwa kwenye Ligi ilikuwa ni katika Msimu wa 2010/11
walipofungwa na Parma Mechi moja kabla Ligi kwisha.
Rekodi ya kutofungwa katika Mechi nyingi inashikiliwa na AC Milan waliyoiweka katika Miaka ya 1990 kwa kutofungwa Mechi 58.
BUNDESLIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Ijumaa Novemba 2
Eintracht Frankfurt v SpVgg Greuther Fürth [Commerzbank-Arena]
Jumamosi Novemba 3
Borussia Dortmund v VfB Stuttgart [Signal-Iduna-Park]
Borussia Monchengladbach v SC Freiburg [Borussia-Park]
Hannover 96 v FC Augsburg [AWD-Arena]
Nurnberg v VfL Wolfsburg [EasyCredit-Stadion]
TSG Hoffenheim v Schalke 04 [Rhein-Neckar-Arena]
Hamburg SV v Bayern Munich [HSH Nordbank Arena]
Jumapili Novemba 4
Bayer Leverkusen v Fortuna Düsseldorf [BayArena]
Werder Bremen v Mainz [Weserstadion]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Vinara wa Bundesliga Bayern Munich
Jumamosi wanatinga kwenye Dabi watakapocheza ugenini na Hamburg kwenye
Mechi ya Ligi ya Bundesliga lakini ndio kwanza wanatoka kwenye kipigo
chao cha kwanza cha Ligi hiyo walipofungwa Wiki iliyopita 2-1 na Bayer
Leverkusen.
Hata hivyo, Bayern, Jumatano, waliichapa Kaiserslautern bao 4-0 katika Mechi ya kugombea German Cup.
Bayern wapo kileleni wakiwa na Pointi 24 wako Pointi 4 mbele ya Schalke na Hamburg wapo nafasi ya 7 wakiwa na Poniti 13.
Schalke watakuwa ugenini kucheza na Timu ya chini Hoffenheim.
Mabingwa watetezi Borussia Dortmund, ambao wapo nafasi ya 4, watacheza Jumamosi na Stuttgart.
LA LIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Jumamosi Novemba 3
Málaga v Rayo Vallecano [Estadio La Rosaleda]
2000 Barcelona v Celta Vigo [Estadio Camp Nou]
2200 Real Madrid v Real Zaragoza [Estadio Santiago Bernabéu]
Jumapili Novemba 4
Deportivo La Coruña v Mallorca [Estadio Riazor]
Granada v Athletic Bilbao [Estadio Los Cármenes]
Osasuna v Valladolid [Estadio El Sadar]
Real Sociedad v Espanyol [Estadio Anoeta]
Sevilla FC v Levante [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
Valencia v Atlético Madrid [Estadio Mestalla]
Jumatatu Novemba 5
Getafe v Real Betis [Coliseum Alfonso Perez]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya kushinda kwenye Mechi zao za
Copa del Rey katikati ya Wiki vinara Barcelona, Timu ya pili Atletico
Madrid na Mabingwa watetezi Real Madrid wote wapo dimbani Wikiendi hii
kucheza Mechi za La Liga.
Barcelona ambao waliwafunga Alaves 3-0
kwenye Mechi ya Copa del Rey na kuwapumzisha Mastaa wao, Kipa Victor
Valdes, Xavi Hernandez, Lionel Messi na Pedro Rodriguez, wanatarajiwa
kuwarudisha wote hao watakapocheza na Celta Vigo Uwanjani Nou Camp.
Atletico Madrid, ambao nao waliipiga Jaen 3-0 kwenye Copa del Rey, wataenda ugenini kucheza na Valencia.
Nao Mabingwa Real Madrid, ambao pia
walishinda kwenye Copa del Rey kwa kuichapa Alcoyano bao 4-1, watakuwa
nyumbani Estadio Santiago Bernabeu kucheza na Real Zaragoza huku
wakijijua wako Pointi 8 nyuma ya Barca na ni lazima wapate matokeo
mazuri.



No comments:
Post a Comment