Sunday, September 23, 2012

Yanga yazinduka yapiga 4, Azam yatungua 1!

!

Jumamosi, 22 Septemba 2012 20:20
Chapisha Toleo la kuchapisha
YANGA_MJENGO>>TAARIFA TFF: Kinamama kuchaguana!
MATOKEO:
Septemba 22
Yanga 4 JKT Ruvu 1
Azam 1 Mtibwa Sugar 0
JKT Oljoro 1 Polisi Morogoro 0
Coastal Union 0 Toto Africans 0
++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya kutoka sare katika Mechi yao ya kwanza na kufungwa iliyofuatia, Yanga leo, kwenye Mechi yao ya 3 ya Ligi Kuu Vodacom, wamezinduka na kuitandika JKT Ruvu bao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa na huko Chamazi wenyeji Azam FC waliifunga Mtibwa Sugar kawa bao 1-0.
Yanga, ambao jana walifuta Mkataba na Kocha wao Tom Saintfiet na leo kuwa chini ya Freddy Felix ‘Minziro’, walianza kupata bao katika Dakika ya 4 tu mfungaji akiwa Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kupata bao la pili katika Dakika ya 31 alilofunga Didier Kavumbangu.
Kipindi cha Pili Yanga waliongeza bao mbili kupitia Simon Msuva, Dakika ya 52 na Didier Kavumbangu, Dakika ya 65.
Bao pekee la JKT Ruvu lilifungwa na Mwaipopo.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Yanga: Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza, Simon Msuva.
JKT Ruvu: Said Mohamed, Kessy Mapande, Stanley Nkomola, Damas Makwaya, Charles Timoth, Ally Khan, Haroun Adolf, Said Ahmedi, Omar Changa, Hussein Bunu, Manyasi
HUKO, Chamazi, Azam FC waliifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 kwa bao la Kipre Tchetche.
+++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA Mechi zijazo:
Septemba 23
Mgambo JKT v Kagera Sugar[Mkwakwani, Tanga]
Simba v Ruvu Shootings [National Stadium, Dar Es Salaam]
African Lyon v Tanzania Prisons [Azam Complex, Dar es Salaam]
+++++++++++++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment