Friday, September 7, 2012

SAFARI BRAZIL 2014 yaanza Ijumaa kwa ULAYA!



Chapisha Toleo la kuchapisha
BRAZIL_2014_ORIJINO11>>NCHI 53 zasaka NAFASI 13 tu!!!
>>MABINGWA Duniani Spain Kundi moja na Belarus, Finland, France, Georgia!!
Barani Ulaya, Ijumaa Septemba 7, wanaanza ile safari yao ndefu ya kufika Brazil Mwaka 2014 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Mechi za kwanza kabisa za Makundi yao 9 ambayo Washindi wake 9 watatinga moja kwa moja Fainali hiyo na Washindi wa Pili 8 Bora watapangwa Mechi 4 za Mchujo kupata Timu 4 zitakazokwenda Fainali.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
Kundi A
Belgium
Croatia
Macedonia
Scotland
Serbia
Wales

Kundi B
Armenia
Bulgaria
Czech Republic
Denmark
Italy
Malta

Kundi C
Austria
Faroe Islands
Germany
Kazakhstan
R. of Ireland
Sweden

Kundi D
Andorra
Estonia
Hungary
Netherlands
Romania
Turkey

Kundi E
Albania
Cyprus
Iceland
Norway
Slovenia
Switzerland

Kundi F
Azerbaijan
Israel
Luxembourg
Northern Ireland
Portugal
Russia

Kundi G
Bosnia and Herzegovina
Greece
Latvia
Liechtenstein
Lithuania
Slovakia

Kundi H
England
Moldova
Montenegro
Poland
San Marino
Ukraine

Kundi I
Belarus
Finland
France
Georgia
Spain


+++++++++++++++++++++++++++++++++++
France, walio Kundi I pamoja na Mabingwa wa Dunia Spain, watakaoanza kwa kucheza na Finland, bila shaka, watataka ushindi ili wapige hatua mbele hasa kwa vile Spain wao hawachezi hiyo kesho Ijumaa.
France wapo chini ya Kocha mpya Didier Deschamps na ameshawaonya Wachezaji wake wabadilike na wawe na nidhamu tofauti na Timu hiyo ilivyofanya kwenye Mashindano mawili makubwa yaliyopita, yale ya Kombe la Dunia Mwaka 2010 na EURO 2012, walipokumbwa na migogoro mikubwa ya utovu wa nidhamu.
Germany watakuwa myumbani kuanza na ‘vibonde’  Faroe Islands kwenye Kundi C na England watakuwa ugenini kuivaa Moldova katika Mechi ya Kundi H.
Italy wao watakuwa huko Sofia kucheza na Wenyeji wao Bulgaria katika Mechi ya Kundi B.
Kufuatia kuondoka kwa Kocha Bert van Marwijk, Netherlands ipo chini ya Louis van Gaal, anaesaidiwa na Mchezaji Veterani wa zamani, Patrick Kluivert [Wote Pichani kulia], na moja ya maamuzi yake makubwa ni uamuzi wake wa Straika yupo aiongoze Nchi hiyo kwenye Mechi zake kati ya Robin van Persie aur Klaas Jan Huntelaar.VAN_GAAL_n_KLUIVERT
Netherlands Ijumaa wanacheza na Timu ngumu Uturuki huko Amsterdam na kufuatia ugenini na Hungary hapo Jumanne zote zikiwa Mechi za Kundi D.
Katika Mechi yao ya mwisho ya Kirafiki, Huntelaar ndie alieanza na Holland wakachapwa 4-2 na Belgium lakini kwa sasa Van Persie ni moto sana hasa baada kufunga Bao 4 katika Mechi mbili zake za mwisho kwa Klabu yake mpya Manchester United.
Akiongelea mjadala huo, Van Persie amesema: “Mie nipo tayari kucheza. Ni juu ya Kocha kuamua nicheze na nicheze pozisheni ipi.”
>>KATI ya Ijumaa na Jumanne Jumla Mechi 76 kuchezwa Duniani kote!!
Mbali ya Bara la Ulaya, pia Mabara ya Marekani ya Kusini, Asia na mengineyo, isipokuwa Afrika itakayokuwa na Mechi za kuwania kuingia Fainali za AFCON 2013 huko Afrika Kusini, yatakuwa na Mechi zao za mchujo kutinga Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
Kati ya Ijumaa na Jumanne, jumla ya Mechi 76 za Mchujo za Kombe la Dunia kuchezwa Duniani kote.
KANDA ya ULAYA
RATIBA
[Saa ni za Bongo]
Ijumaa Septemba 7
19:00 Azerbaijan v Israel [Kundi F]
19:00 Russia v  Northern Ireland [Kundi F]
19:00 Kazakstan v Ireland [Kundi C]
20:00 Liechtenstein v Bosnia And Herzegovina [Kundi G]
20:00 Georgia v Belarus [Kundi I]
21:00 Malta v Armenia [Kundi B]
21:00 Estonia v Romania [Kundi D]
21:15 Croatia v Macedonia [Kundi A]
21:30 Slovenia v Switzerland [Kundi E]
21:30 Netherlands vTurkey [Kundi D]
21:30 Latvia v Greece [Kundi G]
21:30 Andorra v Hungary [Kundi D]
21:30 Finland v France [Kundi I]
21:30 Montenegro v Poland [Kundi H]
21:45 Luxembourg v Portugal [Kundi F]
21:45 Moldova v England [Kundi H]
21:45 Germany v Faroe Islands [Kundi C]
21:45 Iceland v Norway [Kundi E]
21:45 Bulgaria v Italy [Kundi B]
21:45 Wales v Belgium [Kundi A]
22:15 Lithuania v Slovakia [Kundi G]
22:30 Albania v Cyprus [Kundi E]
Jumamosi September 8
17:00 Scotland v Serbia [Kundi A]
21:15 Denmark v Czech Republic [Kundi B]
Jumanne Septemba 11
20:00 Israel v Russia [Kundi F]
20:00 Cyprus v Iceland [Kundi E]
20:30 Romania v Andorra [Kundi D]
20:30 Georgia v Spain [Kundi I]
21:00 Norway v Slovenia [Kundi E]
21:00 Turkey v Estonia [Kundi D]
21:00 Bulgaria v Armenia [Kundi B]
21:15 Bosnia And Herzegovina v Latvia [Kundi G]
21:15 Slovakia v Liechtenstein [Kundi G]
21:30 Austria v Germany [Kundi C]
21:30 Sweden v Kazakstan [Kundi C]
21:30 Hungary v Netherlands [Kundi D]
21:30 San Marino v Montenegro [Kundi H]
21:30 Switzerland v Albania [Kundi E]
21:30 Serbia v Wales [Kundi A]
21:45 Poland v Moldova [Kundi H]
21:45 Northern Ireland v Luxembourg [Kundi F]
21:45 Greece v Lithuania [Kundi G]
21:45 Belgium v Croatia [Kundi A]
21:45 Italy v Malta [Kundi B]
22:00 France v Belarus [Kundi I]
22:00 Scotland v Macedonia [Kundi A]
22:00 England v Ukraine [Kundi H]
23:00 Portugal v Azerbaijan [Kundi F]
KANDA ya MAREKANI ya KUSINI
RATIBA
[Saa ni za Bongo]
Ijumaa Septemba 7
23:30 Colombia v Uruguay
Jumamosi September 8
0:00 Ecuado v Bolivia
2:10 Argentina v Paraguay
4:25 Peru v Venezuela
Jumanne Septemba 11
22:30 Chile v Colombia
Jumatano Septemba 12
0:30 Uruguay v Ecuador
2:25 Paraguay v Venezuela
4:25 Peru v Argentina
MSIMAMO:
1 Chile Mechi 6 Pointi 12
2 Uruguay Mechi 5 Pointi 11
3 Argentina Mechi 5 Pointi 10
4 Ecuador Mechi 5 Pointi 9
5 Venezuela Mechi 6 Pointi 8
5 Colombia Mechi 5 Pointi 7
7 Bolivia Mechi 6 Pointi 4
8 Paraguay Mechi 5 Pointi 4
8 Peru Mechi 5 Pointi 3
FAHAMU: Timu 4 za juu zinatinga Fainali Brazil moja kwa moja na ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo.

No comments:

Post a Comment