Friday, September 7, 2012

Sagna ailipua Arsenal!



Chapisha Toleo la kuchapisha
WENGER-SITABWAGA_MANYANGA>>ASHANGAZWA kuuzwa Song!!
>>AKIRI TAMAA ALIPOWAONA NASRI, CLICHY WAKIBEBA KOMBE!!
Wakati bado yupo majeruhi, lakini anakaribia kuwa fiti, Fulbeki wa Arsenal, Bacary Sagna, ameilipua Klabu yake huko kwao Ufaransa baada ya kutoboa kwa Wanahabari kuwa haelewi, anashangazwa na kukerwa na mambo yanavyotendeka ndani ya Klabu hiyo huku yeye mwenyewe Mkataba wake ukielekea ukingoni bila ya kujua nini kitafuatia.
Sagna, Miaka 29, ambae Mkataba wake utamalizika Mwaka 2014 na ambae amekuwa nje ya Uwanja baada ya kuvunjika mguu, amekiri kuwa na wasiwasi na hali ilivyo ndani ya Emirates na sasa anategemea Wachezaji kuuzwa kila Msimu mpya unapoanza.
Amesema: “Kwa sasa Arsenal, unatoka likizo, unarudi kuanza maandaliza, na unaona Wachezaji wawili wanauzwa na Msimu unaanza! Hivi ndivyo ilivyo tangu nije Klabuni hapa! Tumezoea sasa!”
Aliongeza: “Nilitegemea kuondoka kwa Van Persie. Wote tulitegemea, ilikuwa wazi! Lakini kuondoka kwa Alex Song ndiko kumeshangaza! Bado ana Miaka 24 na ana Miaka mitatu kwenye Mkataba wake! Ni hasara kubwa kwa Klabu kumpoteza!!”
Sagna alisikitika: “Ukiona Wachezaji wenu wazuri wa Msimu uliopita wakiondoka, unajiuliza sana! Wakati mwingine mtaani, Mashabiki wananihoji. Naelewa kwanini wanakasirika! Hata mie nimekasirika! Niko kama wao, sielewi kila kitu”
Sagna pia amekiri yeye ndie Mchezaji pekee wa Kikosi cha Kwanza cha Mwaka 2007 ambae amebaki na amesema: “Mwezi Mei niliwaangalia Man City wakitembeza Kombe! Niliwaona Samir Nasri na Gael Clichy wakibeba Kombe! Hilo limenipa tamaa. Je walikuwa sahihi kuondoka? Ndio. Lakini walipoondoka hatukujua.”
Kuhusu hatima yake, Sagna amesema hajui lolote na mwishoni mwa Msimu huu atabakiza Mwaka mmoja lakini Klabu haijamdokezea chochote.
Pia, Mchezaji huyo amesema ameshaanza mazoezi ya kucheza Mpira baada ya kuvunjika mguu mwishoni mwa Msimu uliopita na anategemea kurejea Uwanjani mara tu baada ya mapumziko ya Mechi za Klabu kwa sasa kupisha Mechi za Kimataifa kumalizika.

No comments:

Post a Comment