Friday, September 7, 2012

OEY BARTON ahamia Ufaransa na Pingu zake!!


Ijumaa, 07 Septemba 2012 06:44
Chapisha Toleo la kuchapisha
JOEY_BARTON_AZUIWA>>LAKINI RUKSA kucheza EUROPA LIGI!!
Joey Barton amehama England kwenda kucheza Ufaransa kwa Mkataba wa mkopo wa Mwaka mmoja lakini Kifungo chake cha Mechi 12 kimeshindwa kukwepeka baada ya Shirikisho la Soka France, LFP, kuthibitisha Mchezaji huyo wa Queens Park Rangers itabidi amalizie adhabu yake iliyobaki ya Mechi 9, baada ya kutumikia adhabu ya Mechi 3, akiwa kwenye Klabu yake mpya Marseille.
Joey Barton, akiwa Nahodha wa QPR siku ya mwisho ya Ligi Kuu England Mwezi Mei wakicheza ugenini Uwanja wa Etihad na Manchester City na kufungwa bao 3-2 zilizowapa Ubingwa Man City, alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu na kuzuka rabsha zilizosababisha Kifungo chake.
Sasa LFP imethibitisha kuwa imepewa taarifa rasmi toka FA, Chama cha Soka England, na adhabu ya Barton itaendelea na atazikosa Mechi za Marseille hadi Novemba 18 ambako Klabu hiyo itacheza na Bordeaux.
LFP imesema, Barton ambae ameshazikosa Mechi 3 za QPR Msimu huu, itabidi akose Mechi 9 za Marseille kwa mujibu wa Sheria za FIFA.
Hata hivyo, Kifungo cha Barton hakihusu Mechi za UEFA na yupo huru kuichezea Klabu yake Marseille hapo Septemba 20 watakapokuwa ugenini kucheza na Fenerbahçe kwenye Mechi ya Kundi C.

No comments:

Post a Comment