Jumatano, 19 Septemba 2012 00:04
UEFA
CHAMPIONZ LIGI imeanza Mechi za Makundi kwa raha tupu kwa baadhi ya
Wadau hasa wale wa Real Madrid baada ya Staa ‘ánaehuzunika’ kufurahi
sana kwa kuwafunga Mahasimu wake wa zamani Manchester City kwa bao la
ushindi la Dakika ya 90 na huyo si mwingine ni Cristiano Ronaldo ambae
aliwapa Real ushindi wa 3-2 juu ya Man City!
TAARIFA KWA UFUPI TU MECHI ZA JUMATANO:
KUNDI A
-GNK Dinamo Zagreb 0 FC Porto 2
Bao za Defour na Gonzalez zimewapa ushindi wa bao 2-0 FC Porto wakiwa ugenini walipocheza na Dinamo Zagreb.
-Paris Saint-Germain FC 4 FC Dynamo Kyiv 1
PSG imeanza kwa kishindo kwa kuitwanga Dynamo Kiev bao 4-1 huku bao zao zikifungwa na Ibrahimovich, Silva, Alex na Pastore.
KUNDI B
-Olympiacos FC 1 FC Schalke 2
Bao la Jan Klaas Huntelaar limewapa ushindi wa ugenini Schalke wa bao 2-1 dhidi ya Klabu ya Ugiriki Olympiacos.
-Montpellier Hérault SC 1 Arsenal FC 2
Wakitoka
nyuma baada ya kufungwa kwa Penati katika Dakika ya 9, Arsenal
walizinduka na kushinda kwa bao 2-1 kwa bao za Lukas Podolski na
Gervinho.
Vikosi:
Montpellier: Jourdren, Bocaly, Yanga M'Biwa, Hilton, Bedimo, Estrada, Saihi, Mounier, Belhanda, Cabella, Camara.
Akiba: Pionnier, Marveaux, Herrera, Congre, Ait-Fana, Stambouli, Jeunechamp.
Arsenal: Mannone, Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Diaby, Arteta, Gervinho, Cazorla, Podolski, Giroud.
Akiba: Shea, Koscielny, Andre Santos, Walcott, Oxlade-Chamberlain, Ramsey,
Coquelin.
Refa: Carlos Velasco Carballo (Spain)
KUNDI C
-Málaga CF 3 FC Zenit St Petersburg 0
Bao mbili za Isco na Saviola zimewapa ushindi Malaga juu ya Zenit St Petersburg.
-AC Milan 0 RSC Anderlecht 0
KUNDI D
-Borussia Dortmund 1 AFC Ajax 0
Bao la Dakika ya 87 la Robert Lewandowski limewapa Borussia Dortmund ushindi wa bao 1-0 walipocheza na Ajax.
-Real Madrid CF 3 Manchester City 2
Bao la Dakika ya 90 la Cristiano Ronaldo
limewapa ushindi Real Madrid wa bao 3-2 dhidi ya Manchester City baada
ya kutoka nyuma mara mbili na kusawazisha huku bao la pili wakifungwa
katika Dakika ya 85 kwa frikiki ya Kolarov iliyombabatiza Xabi Alonso na
kumhadaa Kipa Casillas.
Kinyume
na Mchezo ulivyokwenda wakiwa wamezidiwa sana na ni uhodari wa Kipa Joe
Hart ndio uliwaweka hai, Man City walitangulia kufunga katika Dakika ya
68 kwa bao la Dzeko na Real kurudisha Dakika ya 76 kwa bao la Marcelo.
Vikosi:
Real Madrid: Casillas, Varane, Pepe, Marcelo, Arbeloa, Khedira, Alonso, Essien, Di María, Ronaldo, Higuaín
Akiba: Adan, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Kaka, Benzema, Ozil, Modric.
Manchester City: Hart; Maicon, Kompany, Nastasic, Clichy; Javi Garcia, Barry; Nasri, Yaya Toure, Silva; Tevez.
Akiba: Pantilimon, Lescott, Zabaleta, Kolarov, Rodwell, Aguero, Dzeko
Refa: Damir Skomina (Slovenia)
=====================
RATIBA:
Jumatano Septemba 19
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu]
FC Shakhtar Donetsk v FC Nordsjælland
Chelsea FC v Juventus
LOSC Lille v FC BATE Borisov
FC Bayern München v Valencia CF
FC Barcelona v FC Spartak Moskva
Celtic FC v SL Benfica
Manchester United FC v Galatasaray A.S.
SC Braga v CFR 1907 Cluj



No comments:
Post a Comment