Jumatano, 19 Septemba 2012
>>MAN CITY MTAFARUKU KIGONGO cha RONALDO!!
Meneja wa Manchester City Roberto
Mancini amemtaka Kipa wake awache kuiponda Timu na kumwachia yeye kuwa
ndie ataeihukumu Timu kufuatia kipigo chao cha jana huko Santiago
Bernabeu ambapo Real Madrid walikuwa nyuma kwa bao 2-1 zikiwa zimebaki
Dakika 5 na kuibuka kidedea kwa bao 3-2 huku bao la tatu likifungwa na
Cristiano Ronaldo katika Dakika ya 90.
Mara baada ya Mechi hiyo ya kwanza ya Kundi D la UEFA CHAMPIONZ LIGI,
Kipa wa Man City, Joe Hart, alitamka: “Huwezi kuwa bao 2-1 mbele zikiwa
zimebaki Dakika 5 na kufungwa gemu. Tujilaumu wenyewe. Hatuwezi
kuendelea kuzungumzia uzoefu. Tunao Wachezaji wazuri wanaochezea Timu
zao za Taifa. Wanacheza gemu nyingi sana.”
Kauli hiyo ya Joe Hart imemfanya Roberto
Mancini alipuke na kubatuka: “Kama kuna Mtu anaweza kuiponda Timu basi
ni mimi na si Joe Hart. Joe Hart yeye abaki kuwa Kipa tu. Mie ndio Jaji
na si Joe Hart!”
Kwenye Mechi ya jana, Man City
waliandamwa na kubanwa sana na Real lakini walikuwa wao ndio
waliotangulia kufunga kwa bao la Edin Dzeko.
Marcelo akaisawazishia Real lakini ni
Man City tena waliochukua uongozi kwa bao la frikiki ya Aleksandar
Kolarov katika Dakika ya 85.
Lakini mashuti ya Karim Benzema na Cristiano Ronaldo yaliwapa ushindi Real Madrid.
Mancini aliongeza: “Ni ngumu si kwa
sababu tumefungwa, unaweza kufungwa na Timu kama Real Madrid, lakini
zilibaki Dakika 4 na tulikuwa mbele kwa 2-1. Inashangaza. Inabidi
tujiimarisha zaidi.”
Msimu uliopita Man City ilitolewa nje
kwenye Mashindano haya hatua ya Makundi na Msimu huu Roberto Mancini
anataka waende mbali zaidi.
Amesema: “Tumebakisha Mechi 5 kwenye
Kundi na ni muhimu tuifunge Borussia Dortmund Uwanja wetu wa nyumbani.
Itakuwa vigumu lakini tunataka kusonga mbele.”
=====================
RATIBA-UEFA CHAMPIONZ LIGI:
Jumatano Septemba 19
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu]
FC Shakhtar Donetsk v FC Nordsjælland
Chelsea FC v Juventus
LOSC Lille v FC BATE Borisov
FC Bayern München v Valencia CF
FC Barcelona v FC Spartak Moskva
Celtic FC v SL Benfica
Manchester United FC v Galatasaray A.S.
SC Braga v CFR 1907 Cluj



No comments:
Post a Comment