Jumatano, 19 Septemba 2012 1
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI YA TFF:
Release No. 149
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Septemba 19, 2012
KLABU LIGI KUU, WADHAMINI VODACOM KUTETA
Klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom zimekubaliana kukutana na mdhamini (kampuni ya simu za mkononi
ya Vodacom) kuzungumzia kipengele cha mkataba wa ligi hiyo kinachozuia
kampuni nyingine za mawasiliano kudhamini timu zinazocheza Ligi Kuu.
Maazimio hayo
yalifikiwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika kikao kati ya klabu hizo
na Kamati ya Ligi kilichofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wallace Karia.
Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.
Maazimio mengine ya
kikao hicho ni TFF kuiandikia barua African Lyon ambayo itaipeleka kwa
mdhamini wake (Zantel) ikielezea hatua hiyo ili kusimamisha udhamini huo
wakati ikisubiri matokeo ya mazungumzo kati ya klabu hizo na mdhamini
wa Ligi Kuu juu ya kipengele cha kuzuia washindani wa Vodacom.
Katika mkutano huo,
watendaji wawili wa Kamati ya Ligi ambayo iko katika kipindi cha mpito
kuelekea kuundwa kwa Bodi ya Ligi walitambulishwa kwa klabu hizo.
Watendaji hao ni Silas Mwakibinga ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) na
Joel Balisidya ambaye ni Ofisa wa Ligi (LO).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF



No comments:
Post a Comment