Wednesday, September 19, 2012

SHIREFA MKOA WA SHINYANGA KIZUNGUZUNGU

kamati ya utendaji ya shirefa iliyokutana tarehe 14/9/2012 imemsimamisha uongozi hadi mkutano mkuu utakapo kutana mwenyekiti wa shirefa mkoa mkoa wa shinyanga ndugu benenesta rugora

 kamati hiyo imetoa maamuzi hayo kutokana na hatua za kinidhamu kutokana na makosa aliyo ya fanya  mwaka 2009 bila idhini ya kamati ya utendaji kuchukua fedha ya chama Tsh 600,00/= zilizo tolewa na NMB kwa ajili ya kozi ya awari ya makocha fadha hizo hazijarudishwa

pia kamati hiyo imebainisha kuwa mwaka 2010 mwenyekiti huyo alitumwa na kamati ya utendaji kwenda Dar es salaam kufuata fedha za fidia ya Shirefa kutoka clabu ya simba jumla ya Tsh 5,400,00/= toka kipindi hicho fedha hiyo hajaikabidhi  Shirefa na kusababisha  shirefa kuingia kwenye madeni na mahusiano mabaya na jamii .

kwa mjibu wa kamati kutokana na makosa hayo pamoja na tabia hiyo isiyo njema ya kutumia fedha za chama bila idhini kamati hiyo iliamua kumsimamisha ; hadi maamuzi ya mkutano mkuu wa shirefa mkoa wa shinyanga

barua hiyo imesainiwa na Ibrahimu  magoma  katibu mkuu wa shirefa

No comments:

Post a Comment