Saturday, September 8, 2012

FIFA yagoma Odjidja-Ofoe kutua Everton!

 

Jumamosi, 08 Septemba 2012 08:19
Chapisha Toleo la kuchapisha
PHILLIP_NEVILLEMpango wa Everton kumsajili Kiungo Vadis Odjidja-Ofoe kutoka Club Brugge umepiga mwamba baada ya FIFA kugoma kuubariki.
Everton walikamilisha dili ya kumchukua kwa mkopo Vadis Odjidja-Ofoe Wiki moja iliyopita na waliwasilisha Makabrasha ya Uhamisho huo kabla Dirisha la Uhamisho wa Wachezaji kufungwa Ijumaa Agosti 31 lakini Uhamisho huo pia ulihitaji baraka za FIFA.
++++++++++++++++++++++
NI NANI Vadis Odjidja-Ofoe?
  • UMRI: 23
  • NAFASI: Kiungo
  • KLABU ALIZOCHEZA: Anderlecht, Hamburg, Club Brugge
  • MECHI TIMU ya TAIFA: Belgium 3
++++++++++++++++++++++
Kugomewa huko na FIFA kumetangazwa na Everton ambao wamesema licha ya wao kupata baraka zote za Uhamisho huo kutoka kwa Chama cha Soka England, FA, na Wasimamizi wa Ligi Kuu England huku Everton wakiwasilisha Makabrasha ya Mchezaji huyo katika muda muafaka, FIFA imekataa kumruhusu Mchezaji huyo kucheza Goodison Park.
Everton imesema inatafakari njia zote ili kuamua nini wakifanye.
Everton, iliyo chini ya Meneja David Moyes na Nahodha Phllip Neville, ni Klabu ambayo haina Wachezaji wengi wa Kikosi cha Kwanza na Miaka nenda rudi wamekuwa wakikabiliwa na ukata wa kununua Wachezaji.

No comments:

Post a Comment