Jumamosi, 08 Septemba 2012 08:46

>>OX nae asifiwa!!
Meneja wa Timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson, pamoja na Mkongwe wa Timu hiyo, Frank Lampard, wamemmwagia sifa Kiungo Tom Cleverley kwa umiliki wake wa nafasi hiyo kwenye Mechi na Moldova iliyochezwa huko Chisinau hapo jana na England kushinda bao 5-0 katika Mechi yake ya kwanza ya Kundi H kuwania kwenda Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
Akiichezea England Mechi yake ya pili tu, Cleverley, Miaka 23, Kiungo huyo wa Manchester United alianzishwa badala ya mwenzake wa Klabu moja Michael Carrick na kuwa pamoja kwenye nafasi hiyo na Frank Lampard na Steve Gerrard ambe alitolewa baada ya Dakika 45 na kuingizwa Carrick.
Hodgson alisema: “Alicheza vizuri sana Dakika zote 90 na ukitazama utajua kwa nini Sir Alex Ferguson anafurahishwa na Mchezaji huyu!”
Nae Mkongwe Lampard, ambae jana alifunga Bao mbili, amesema: “Ni furaha kucheza na Tom na bado yu Kijana hivi atakuwemo kwenye Timu hii kwa Miaka mingi tu.”
Mbali ya kufurahishwa na Cleverley, pia Hodgson alifurahishwa na Winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain ambae alicheza kwa Dakika 60 na kutolewa na nafasi yake kushikwa na mwenzake wa Arsenal Theo Walcott.
Jumanne ijayo England itakuwepo Uwanja wa Wembley Jijini London kucheza na Ukraine katika Mechi yake ya pili ya Kundi H kuwania kwenda Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
No comments:
Post a Comment