Jumamosi, 01 Septemba 2012 12:15
>>SIR ALEX FERGUSON KUWEKA REKODI=MECHI 1000 za LIGI!!>>BIGI MECHI ni Jumapili: Liverpool v Arsenal
+++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Septemba 1
[Bongo Taimu]
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
West Ham United v Fulham
[Saa 11 Jioni]
Swansea City v Sunderland
Tottenham Hotspur v Norwich City
West Bromwich Albion v Everton
Wigan Athletic v Stoke City
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Manchester City v Queens Park Rangers
Jumapili Septemba 2
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Liverpool v Arsenal
[Saa 12 Jioni]
Newcastle United v Aston Villa
Southampton v Manchester United
TAARIFA:
Dirisha la Uhamisho kwa Majira haya ya Joto limefungwa jana Usiku na litafunguliwa tena Januari Mosi na sasa hamna tena visingizio toka kwa Mameneja kuwa wanahitaji Wachezaji wapya kuongezea nguvu Timu na badala yake wachezeshe waliokuwa nao tu.
+++++++++++++++++++++++++++++
SIR ALEX FERGUSON====REKODI

MECHI 999:
Ushindi: 598
Sare: 233
Kufungwa: 168
+++++++++++++++++++++++++++++
Jumamosi na Jumapili zipo Mechi 9 za Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League], lakini ‘BIGI MECHI’, bila shaka, ni ile ya Jumapili huko Anfield kati ya Liverpool na Arsenal.
Wiki iliyopita, Uwanjani Anfield, Liverpool walitoka sare 2-2 na Mabingwa watetezi Manchester City.
IFUATAYO ni TATHMINI fupi ya kila Mechi:
JUMAMOSI
Manchester City v QPR
Kati ya Mechi mbili za Ligi walizocheza Msimu huu, Manchester City wameshinda moja, kwa taabu 3-2 na Southampton, na kutoka sare 2-2 na Liverpool huku baadhi ya Wachezaji wao wakionyesha kufifia.
Ukimwondoa mpiganaji Yaya Toure, wengine kama David Silva, wanaonekana kupwaya.
QPR wamempata Kiungo mzuri, Esteban Granero, kutoka Real Madrid, na pengine ataibeba Timu hii ambayo ilianza Ligi kwa kichapo cha nyumbani cha Bao 5-0 mikononi mwa Swansea lakini wakazinduka na kutoka sare ya Bao 1-1 ugenini na Norwich City.
West Ham v Fulham
Je West Ham watamwanzisha Straika wao mpya Andy Carroll waliemkopa kutoka Liverpool?
Fulham, walioanza Ligi kwa ushindi wa bao 5-0 dhidi ya Norwich City na kufungwa 3-2 na Manchester United Uwanjani Old Trafford, ni Timu ngumu lakini West Ham, chini ya Meneja Sam Allardyce na Nahodha Kevin Nolan, ni Timu ngumu pia hasa ikiwa kwao Upton Park.
Swansea v Sunderland
Hii inategemewa kuwa Mechi tamu ya Soka linalotandazwa chini ndani ya Liberty Stadium na vita itakuwa kwenye Kiungo kati ya Leon Britton wa Swansea na Stephane Sessegnon wa Sunderland.
Sunderland huenda wakamwanzisha Winga Adam Johnson waliemnunua kutoka Manchester City.
Tottenham v Norwich
Hii ni Mechi ambayo huenda Wachezaji wapya wakaipamba kwa Sebastien Bassong, alietoka Tottenham, kuichezea Norwich, na Emmanuel Adebayor kuichezea Tottenham kwa mara ya kwanza baada ya kuhamishwa rasmi kutoka Man City huku Kiungo mpya wa Tottenham Moussa Dembele akijaribu kuvaa viatu vilivyoachwa na Luka Modric aliehamia Real Madrid.
Kwa Meneja mpya wa Tottenham, Andre Villas-Boas, ushindi kwenye Mechi hii ni lazima hasa baada ya kuanza Ligi kwa kuchapwa 2-1 na Newcastle na kutoka sare 1-1 na WBA.
West Brom v Everton
West Bromwich na Everton zote zimeanza vizuri, kwa WBA kuichapa Liverpool 3-0 na kwenda sare na Tottenham na Everton kushinda Mechi zao zote mbili, 1-0 dhidi ya Man United na 3-1 dhidi ya Aston Villa.
Mechi hii inategemewa kuwa ni vita ya angani kati ya Jonas Olsson na Marouane Fellaini.
Wigan v Stoke
Stoke, wanaotegemea miguvu si kasi, sasa wanae Arouna Kone ambae atapambana na Ryan Shawcross huku akisaidiwa na Peter Crouch.
Stoke wameimarisha Kiungo chao kwa kumnunua Charlie Adam kutoka Liverpool.
Liverpool v Arsenal
Hii ni BIGI MECHI kati ya Timu mbili ambazo hazijashinda Msimu huu.
Msimu uliopita Liverpool walifungwa nad Arsenal Bao 2-1, kwa bao za Robin van Persie, lakini safari hii Van Persie yupo Man United na itabidi wawategemee Wachezaji wao wapya, Lukas Podolski na Olivier Giroud, kuwapa Magoli.
Mechi hii, kwenye Winga moja, itawakutanisha Vijana wapya hatari, Winga mdogo wa Liverpool, Raheem Sterling, atakaepambana na Beki chipukizi Carl Jenkinson.
Hii ni Mechi nzuri na pengine Arsenal wataziona nyavu kwa mara ya kwanza Msimu huu baada ya kutoka sare za 0-0 katika Mechi zao mbili za kwanza huku Liverpool wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kufungwa na kutoka sare katika Mechi zao.
Newcastle v Aston Villa
Aston Villa inategemewa kumuanzisha Mchezaji mpya Charles N'Zogbia ambae ni hatari kwa mashuti ya mbali.
Wakati Aston Villa wameanza Msimu huu kwa vichapo viwili mfululizo, Newcastle wao wameshinda moja na kufungwa moja na hii italeta mvutano mkubwa kwenye Mechi ambayo inaweza kuzaa lundo la Magoli hasa kwa vile wapo Wafungaji hatari kina Demba Ba na Cisse kwa Newcastle.
Southampton v Manchester United
Sir Alex Ferguson anaingia kwenye Mechi hii akitazamiwa kuweka rekodi mpya ya kuwa Meneja katika Mechi 1,000 za Ligi baada ya kumaliza kusimamia Mechi 999 hivi juzi.
Manchester United itacheza bila majeruhi Wayne Rooney na Ashley Young lakini itampata Jonny Evans ambae amepona na huenda akacheza kama Sentahafu na hivyo kuruhusu Michael Carrick acheze Kiungo badala ya Sentahafu kama alivyocheza katika Mechi mbili zilizopita.
Southampton wanaweza kuwachezesha Wachezaji wao wapya wawili, Mjapan Maya Yoshida na Mzambia Emmanuel Mayuka, huku mbele wakimweka Rickie Lambert ili kuwapatia mabao.
Katika Miaka ya nyuma Southampton wamekuwa kikwazo kikubwa kwa Man United na ukiangalia Mechi zao mbili za Ligi Msimu huu, walipofungwa 3-2 na Man City na 2-0 na Wigan, utakubali ni Timu ngumu licha ya vipigo hivyo.



No comments:
Post a Comment