Jumamosi, 01 Septemba 2012 14:25
Klabu ya Italy Fiorentina imelipuka kwa hasira baada ya kumkosa aliekuwa Straika wa Manchester United Dimitar Berbatov ambae walifikia makubaliano ajiunge nao Siku ya Jumatano lakini katika Dakika za mwisho akaingia mitini wakati Mamia ya Mashabiki wa Timu hiyo pamoja na Mkurugenzi wa Klabu Eduardo Macia wakimngojea kumpokea Uwanja wa Ndege wa Mji wa Florence huku kwenye Ofisi za Klabu Mkurugenzi mwingine, Daniele Prade, akisubiri na Mkataba wa Miaka miwili.Wakitoa taarifa, Fiorentina wamedai Mchezaji huyo na Wakala wake walitumiwa Tiketi ya Ndege lakini Klabu nyingine zenye uroho ziliingilia kati huku wao wakiinyoshea kidole Juventus.
Lakini, hata hivyo, Mchezaji huyo jana alikamilisha Usajili kwenye Klabu ya London, Fulham, ambayo nako amepewa Mkataba wa Miaka miwili.
Fiorentina imetamka kwa hasira: “Berbatov hastahili Mji wetu, Jezi yetu na thamani yake inayowakilisha!”
Kocha wa Juve Antonio Conte
Kocha wa Juventus Antonio Conte amekata Rufaa kwa mara ya pili akipinga adhabu ya kufungiwa Miezi 10 na Shirikisho la Soka Italy, FIGC, na hii ni nafasi yake ya mwisho kukwepa adhabu hii aliyopewa kwa kuhusishwa na upangaji matokeo Mechi wakati akiwa na Klabu ya Serie B Siena katika Msimu wa Mwaka 2010/11.
Conte ametaka Rufaa hii, ambayo itasikilizwa na Shirikisho la Michezo la Italy, CONI, iisikilize haraka na pia Kifungo chake kisimamishwe wakati Rufaa yake inaendelea kusikilizwa.



No comments:
Post a Comment