Jumamosi, 01 Septemba 2012 16:51
>>WAPYA Berba, Richardson, Carroll wacheza!Andy Carroll, akiichezea Timu yake mpya West Ham kwa mara ya kwanza, alitengeneza bao mbili

Wakati West Ham walipoichapa Fulham bao 3-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, BPL, iliyochezwa leo Uwanja wa Upton Park.
Bao zote 3 zilifungwa Kipindi cha Kwanza.
Bao la kwanza la West Ham lilifungwa katika Sekunde ya 53 toka Mechi ianze baada ya pasi ya Carroll kumfikia Ricardo Vaz Te aliemsogezea Nahodha Kevin Nolan aliefunga kwa kigongo kikali.
+++++++++++++++++++++++++MAGOLI:
West Ham:
-Kevin Nolan, Dakika ya 1
-Winston Reid, 29
-Matt Taylor, 41
+++++++++++++++++++++++++
Goli la pili la Fulham lilitokana na kona huku Difensi yote ya Fulham ikimzonga Andy Carroll lakini ni Winston Reid ndie aliefunga kwa kichwa cha nguvu.
Hata goli la tatu lilitokana na Difensi ya Fulham kumjali Carroll na kumpa mwanya Matt Taylor kuachia shuti la chini ambalo Kipa Mark Scwarzer alishindwa kudaka.
Katika Mechi hii, Wachezaji wapya, Kieran Richardson na Dimitar Berbatov kwa Fulham, walicheza Mechi zao za kwanza na Richarson alianza Kipindi cha Kwanza na kutolewa Kipindi cha Pili wakati Berbatov aliingizwa Kipindi cha Pili.
VIKOSI:
West Ham United: Jaaskelainen, Demel, Reid, Collins, O'Brien, Noble, Diame, Nolan, Vaz Te, Taylor, Carroll
Akiba: Henderson, Tomkins, Diarra, O'Neil, Maiga, Hall, Cole
Fulham: Schwarzer, Riether, Hangeland, Hughes, Riise, Diarra, Sidwell, Richardson, Duff, Rodallega, Petric
Akiba: Stockdale, Kelly, Baird, Kasami, Berbatov, Briggs, Kacaniklic



No comments:
Post a Comment