Ijumaa, 02 Novemba 2012 01:49
>>OLD TRAFFORD Jumamosi: Man United v Arsenal!
>>MECHI ya kwanza Robin van Persie kukutana na Ze Ganaz tangu ahame!!
>>WENGER aungama: “RVP ni Denja!!”
Arsene Wenger amepoza maneno ya Mashabiki wa Arsenal kutaka kisasi kwa Robin van Persie kwa
kuihama
Timu hiyo na kwenda Manchester United wakati Timu hizo zitakapokutana
Jumamosi Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na hiyo
ikiwa mara ya kwanza kwa Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kukutana na
Timu yake ya zamani tangu ahame.
Wenger amewataka Mashabiki wa Arsenal
watakaokuwepo Old Trafford kumwonyeshea heshima Robin van Persie na si
kumkashifu na kumtukana.
Wenger alitamka: “Kwetu, muhimu ni
matokeo na uchezaji wetu. Hatumzunguzii kabisa Van Persie. Natumaini
Mashabiki watamuheshimu kwani kachezea kwetu Miaka minane na alifanya
vizuri sana!”
Alihoji: “Tunapiga vita Ubaguzi, Wiki iliyopita ilikuwa hivyo na kwa nini isiwe sasa?”
Akiichezea Arsenal, Robin van Persie,
mwenye Miaka 29, aliifungia Arsenal jumla ya Mabao 132, 37 yakiwa Msimu
uliopita na kuwawezesha kushika nafasi ya 3 kwenye Ligi.
Wenger amesema: “Daima unataka uongoze
Watu vizuri wawe na maisha mazuri! Wakifanikiwa unaridhika, sidhani
kwake nilifanya vibaya!”
Hadi sasa, kwa Kipindi kifupi, Van
Persie ameifungia Man United Bao 7 kwenye Ligi na yeye na Demba Ba wa
Newcastle ndio wanaongoza kwenye Ufungaji.
Hilo halikumshangaza Wenger ambae
ametamka: “Sishangazwi na yeye kufanya vizuri. Man United ina Wachezaji
wazuri sana, na Robin ni mjanja kwenye boksi, mwenye kasi na kujua
nafasi huashangaza! Wapo Wachezaji wazuri na Robin atanufaika tu. Robin
ni Straika hatari sana!”



No comments:
Post a Comment