Thursday, September 6, 2012

UDHAMINI MPYA LIGI KUU KUANIKWA SOON



Simba na Azam zitafungua pazi la Ligi Kuu Jumanne ijayo kwa mechi ya Ngao ya Jamii

MKATABA wa udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itadhaminiwa tena Vodacom utasainiwa Jumanne (Septemba 11 mwaka huu) kwenye ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Shiriksiho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo, ameiambia dimbani leo, leo kwamba taarifa rasmi juu ya muda wa kusaini na pande zitakazoshuhudia hafla hiyo itatolewa hivi karibuni.
Msimu mpya wa Ligi Kuu, 2012/2013 utaanza Septemba 15, mwaka huu kwa timu zote 14 kujitupa kwenye viwanja tofauti.
Mechi za ufunguzi zitakuwa kati ya Simba vs African Lyon (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Polisi Morogoro vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro), Tanzania Prisons vs Yanga (Sokoine, Mbeya), Mgambo JKT vs Coastal Union (Mkwakwani, Tanga), JKT Ruvu vs Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Kagera Sugar vs Azam (Kaitaba, Bukoba) na Toto Africans vs Oljoro JKT (Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa kwanza (first round) utamalizika Novemba 11 mwaka huu ambapo kwenye mzunguko huo mechi ya watani wa jadi Yanga na Simba itachezwa Oktoba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa mechi kati ya Toto Africans vs Ruvu Shooting (Kirumba), Mgambo JKT vs African Lyon (Mkwakwani), JKT Ruvu vs Mtibwa Sugar (Azam Complex), Tanzania Prisons vs Kagera Sugar (Sokoine), Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Azam (Sheikh Amri Abeid Kaluta) na Polisi Morogoro vs Coastal Union (Jamhuri).
Endapo Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.
Wakati huo huo: Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria ufunguzi rasmi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 kati ya bingwa mtetezi Simba na makamu bingwa Azam itachezwa Septemba 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment