Alhamisi, 06 Septemba 2012 10:19

Kocha wa England Roy Hodgson anazidi kukabiliwa na kujiondoa kwa Wachezaji kwa kuumia kwenye Kikosi chake ambacho Ijumaa kinacheza ugenini huko Chisinau na Moldova kwenye Mechi ya Kundi H kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil.
+++++++++++++++++
Kundi H
England
Moldova
Montenegro
Poland
San Marino
Ukraine
+++++++++++++++++
Leo hii msafara wa England utaelekea huko Moldova bila ya Adam Johnson wa Sunderland ambae ameumia pajani mazoezini na huyu anafuatia kujitoa kwa Andy Carroll na Ashley Cole wote baada ya kuumia mara baada ya kuitwa Kikosini. Mara baada ya Mechi ya Ijumaa na Moldova England watarudi kwao kujitayarisha kwa Mechi nyingine ya Kundi H la Kombe la Dunia hapo Septemba 11 watakapokuwa kwao Uwanja wa Wembley Jijini London kucheza na Ukraine. +++++++++++++++++ KIKOSI KILICHOITWA: Makipa: Jack Butland (Birmingham City), Joe Hart (Manchester City), John Ruddy (Norwich City). Mabeki: Leighton Baines (Everton), Ryan Bertrand (Chelsea), Gary Cahill (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Joleon Lescott (Manchester City), John Terry (Chelsea), Kyle Walker (Tottenham Hotspur). Viungo: Michael Carrick (Manchester United), Tom Cleverley (Manchester United), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Steven Gerrard (Liverpool), Adam Johnson (Sunderland), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Theo Walcott (Arsenal). Mafowadi: Andy Carroll (Liverpool), Jermain Defoe (Tottenham Hotspur), Daniel Sturridge (Chelsea), Danny Welbeck (Manchester United). +++++++++++++++++ Licha ya kuondoka kwa Wachezaji hao watatu, Kocha Hodgson hajamwita Mchezaji yeyote kuchukua nafasi zao na amebaki na Wachezaji 21 kwenye Kikosi chake. Mbali ya kukabiliwa na upungufu huo wa Wachezaji wakiwemo Wachezaji wa Manchester United, Wayne Rooney na Ashley Young, ambao hawakuitwa kabisa kwa vile walikuwa wameshaumia, England pia itakabiliwa na hali ngumu ndani ya Uwanja wa Zimbru ambao ni mdogo unaochukua Watu 10,400 wenye miundo mbinu hafifu na pia Kiwanja chake cha kuchezea hakina ubora uliozoeleka na Wachezaji wa England. Moldova, moja ya Nchi masikini huko Ulaya, ipo nafasi ya 48 kwa Ubora kati ya Nchi 53 Wanachama wa UEFA lakini ni wagumu kufungika wakiwa kwao kama walivyoona Holland ambao walishinda kwa taabu Uwanjani Zimbru katika Mechi za mchujo za EURO 2012. Mara ya mwisho kwa England kucheza na Moldova ilikuwa Mwaka 1996 katika Mechi ambayo ndio ilikuwa ya kwanza kabisa kwa David Beckham kuichezea England, Mechi ambayo England walishinda Bao 3-0 kwa bao za Nick Barmby, Paul Gascoigne na Alan Shearer. Mbali ya udhaifu wa dhahiri wa Moldova, Kocha Roy Hodgson, ametoa tahadhari: “Kuna vitu vingi vya kutazamwa ukija sehemu kama hii Moldova. Lazima ukubali Uwanja ulivyo, Kiwanja cha kuchezea kilivyo, mazingira yote na ubora wa wapinzani. Tunajua Watu wanadhani Moldova ni dhaifu lakini sie hatufikirii hiyo.” |
No comments:
Post a Comment