WENGER: “TUNAWEZA KUMALIZA LIGI NAFASI YA 2!!”
>>MECHI INAYOFATA DABI YA LONDON KASKAZINI: SPURS v ARSENAL!!
LICHA YA KUWA POINTI 9 nyuma ya Timu
iliyo nafasi ya Pili, Manchester City, kwenye Msimamo wa Ligi Kuu
England wakiwa nafasi ya 5 huku Mechi zimebaki 11, Meneja wa Arsenal,
Arsene Wenger, amesema kumaliza Ligi nafasi ya Pili haipo nje ya uwezo
wao.
Hivi karibuni Arsenal ilitolewa nje ya
FA CUP na Blackburn Rovers na pia kufungwa na Bayern Munich kwenye UEFA
CHAMPIONZ LIGI lakini Wenger ametamka: “Man City hawako mbali, nje ya
uwezo wetu. Yatakuwa mapigano makali mpaka mwisho!”
++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 27 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Pointi 68
2 Man City 56
3 Chelsea 49
4 Tottenham Mechi 26 Pointi 48
5 Arsenal 47
6 Everton 42
7 WBA 37
++++++++++++++++++++++
Baada ya Wiki ngumu ya vichapo viwili
mfululizo, Arsenal walijikongoja hapo Jumamosi na kuichapa Aston Villa
2-1 kwenye Mechi ya Ligi huo ukiwa ushindi wao wa 3 mfululizo kwenye
Ligi baada ya kuzichapa Sunderland na Stoke City.
Lakini bado wako nafasi ya 5 wakiwa
nyuma ya Vinara Man United, Man City, Chelsea na Tottenham huku
wakikabiliwa na Dabi ya London ya Kaskazini huko Uwanjani White Hart
Lane hapo Machi 3.
++++++++++++++++++++++
MECHI NGUMU KUWANIA NAFASI YA PILI:
|
|
|
|
FAHAMU: A=Ugenini H=Nyumbani
++++++++++++++++++++++
Jumatatu
Usiku, Tottenham watakuwa ugenini huko Upton Park kucheza na West Ham
na ushindi kwao utawafanya waipiku Chelsea toka nafasi ya 3 na kuwa
Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Man City.
Vinara Man United, ambao watacheza na Arsenal hapo Aprili 28 Uwanjani Emirates, wapo Pointi 21 mbele ya Arsenal.
Wakati huo huo, Meneja wa Chelsea Rafael
Benitez amedokeza kufungwa kwao huko Etihad 2-0 na Man City hapo jana
kumewafanya washindwe kuwania kumaliza nafasi mbili za juu na sasa vita
iliyobaki kwao ni kugombea 4 bora.
Nae Wenger bado anayo imani kuwa Arsenal
itazipiku Tottenham na Chelsea na pia Man City pale aliposema: “Si
kupigana na Spurs tu, sidhani kama nafasi nyingine ziko nje ya uwezo
wetu.”
Arsenal, ambao hawajawahi kumaliza Ligi
bila kuwa katika 4 bora tangu Wenger aanze kazi Septemba 1996, mara ya
mwisho kumaliza wakiwa ndani ya Timu mbili za juu ni Msimu wa Mwaka
2004/05 walipotwaa nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Chelsea.
TANGU WATWAE UBINGWA MSIMU WA 2003/04 NAFASI WALIZOMALIZA:
2011-12: Wa 3 Pointi 70
2010-11: Wa 4 Pointi 68
2009-10: Wa 3 Pointi 75
2008-09: Wa 4 Pointi 72
2007-08: Wa 3 Pointi 83
2006-07: Wa 4 Pointi 68
2005-06: Wa 4 Pointi 67
2004-05: Wa 2 Pointi 83
++++++++++++++++++++++
RATIBA
BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumatatu Februari 25
[Saa 5 Usiku]
West Ham United v Tottenham Hotspur
Jumamosi Machi 2
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v West Bromwich Albion
Everton v Reading
Manchester United v Norwich City
Southampton v Queens Park Rangers
Stoke City v West Ham United
Sunderland v Fulham
Swansea City v Newcastle United
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Wigan Athletic v Liverpool
Jumapili Machi 3
[Saa 1 Usiku]
Tottenham Hotspur v Arsenal
Jumatatu Machi 4
[Saa 5 Usiku]
Aston Villa v Manchester City
++++++++++++++++++++++
No comments:
Post a Comment