TAARIFA KWA UMMA
FEBRUARY 6, 2013DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa unyoya (Featherweight) Ramadhani Shauri amepewa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa IBF kwa vijana walio chini ya miaka 25 uzito wa Lightweight. Shauri ambaye alishinda taji la ubingwa wa IBF katika bara la Afrika mwaka jana baada ya kumpiga bondia Sunday Kizito wa Uganda ana rekodi ya mapambano 17.
IBF imeamua kumpatia Shauri
nafasi ya kugombea ubingwa huo wa dunia kwa vijana baada ya kuangalia
mkanda wa video wa pambano lake la ubingwa wa Afrika na kuridhika kuwa
anaweza kushindania ubingwa huo wa vijana,
Mabondia
wengi wa Marekani ambao walikuja kuwa mabingwa wa dunia na kuweza
kupata pesa nyingi walianza kuwa mabingwa wa dunia kwa vijana na hivyo
kuweza kupanda chati kwenye viwango vya IBF. Mbondia hao ni kama Bernard
Hopkins, Floyd Maywealther na Oscar De la Hoya.
Kama
Shauri atashinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa vijana atakuwa
kwenye macho ya mapromota wakubwa duniani kama kina Dong King, Bob Arum
na wengine wengi. Nafasi kama hii inaipa nchi ya Tanzania nafasi nzuri
sana ya kujitangaza kibiashara na utalii kwani dunia inaiona kuwa kati
ya nchi zinazotoa mabingwa wa dunia.
Kama
Shauri atashinda taji hili atakuwa Mtanzania wa kwanza tangu historia
ya ngumi nchini kuweza kushinda taji la shirikisho kubwa kati ya manne
duniana ambayo ni IBF, WBA, WBO na WBA.
Shiriksiho
la Ngumi la Kimatafia Afrika (IBF/Africa) ambalo lina makao yake makuu
ya kuhudumia bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ndilo
lililomtafutia Shauri nafasi aliyopata.
IBF/Africa
inawahamasisha Watanzania walio na mapenzi mema na nchi yao pamoja na
makampuni mbalimbali bifsi ya umma yajitokeze kwa wingi kumpatia Shauri
ufadhili wa kuweza kuligombea taji hili.
Mungu mbariki bondia Ramadhani Shauri, Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amen.
Imetolewa na:
UTAWALA
Shiriklisho la Ngumi la Kimataifa Afrika (IBF/Africa)Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment