>>BIG SAM ADOKEZA: ‘MSIMAMISHE BALE, UMEISIMAMISHA SPURS!’
UWANJA: Upton Park
TAREHE: Jumatatu Februari 25
SAA: 5 Usiku [Bongo Taimu]
+++++++++++++++++++
LEO,
Tottenham wanaingia Upton Park kucheza na West Ham katika Mechi pekee
ya BPL, Barclays Premier League, na ushindi kwao utawafanya waipiku
Chelsea kutoka nafasi ya 3 ya Msimamo wa Ligi.
ZIFUATAZO NI TAARIFA FUPI KUHUSU MECHI HII:
HALI za WACHEZAJI
Majeruhi wa West Ham, Mabeki James Collins na Joey O'Brien, wamesharudi mazoezini na huenda leo wakacheza.
Kipa wa Tottenham Hugo Lloris, ambae ni
Nambari Wani ya France, leo atakaa golini baada ya kupumzishwa kwenye
Mechi ya EUROPA LIGI iliyochezwa Alhamisi walipotoka sare na Lyon.
Majeruhi wa Tottenham ni walewale wa
kitambo ambao ni Straika Jermain Defoe (enka), Younes Kaboul, Sandro na
Tom Huddlestone (Wote goti) na wote hawatacheza.
+++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Mechi 27 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Pointi 68
2 Man City 56
3 Chelsea 49
4 Tottenham Mechi 26 Pointi 48
5 Arsenal 47
6 Everton 42
7 West Brom 40
8 Liverpool 39
9 Swansea 37
10 Stoke 33
11 Fulham 32
12 Norwich 32
13 West Ham Mechi 26 Pointi 30
14 Newcastle 30
15 Sunderland 29
16 Southampton 27
17 Wigan 24
+++++++++++++++++++
18 Aston Villa 24
19 Reading 23
20 QPR 17
+++++++++++++++++++
TATHMINI ya MECHI:
Akikiri kuwa Tottenham inamtegemea sana
Gareth Bale, Meneja wa West Ham kumkosa Jermaine Defoe kumewafanya
wamtegemee Bale hasa kwa vile Straika wao mwingine Emmanuel Adebayor
ndio kwanza amerudi kutoka Afrika Kusini alikokuwa kwenye AFCON 2013 na
Nchi yake Togo.
Bale ameifungia Spurs Mabao katika Mechi 3 za mwisho za Ligi na sasa amefikisha Bao 17.
Allardyce amedokeza kuwa ukimsimamisha Bale, umeisimamisha Spurs.
USO kwa USO:
-Mwanzoni mwa Msimu, West Ham ilichapwa
3-1 na Tottenham Uwanjani White Hart Lane na hiyo ilikuwa Mechi yao ya
11 Uwanjani hapo bila ushindi.
-Katika Mechi 11 za Ligi zilizopita, West Ham wameshinda mara moja tu kwa Bao 1-0, Septemba 2010 kwa Bao la Frederic Piquionne.
-Mechi hii itakuwa ya 137 kukutana na Tottenham wameshinda mara 58 na West Ham mara 44.
REKODI:
West Ham
-West Ham hawajafungwa katika Mechi 3 za Ligi walizocheza nyumbani na wamezifunga Swansea na Norwich na kutoka Droo 1-1 na QPR.
-Kevin Nolan ndie Mfungaji wao bora na hadi sasa ameifungia Bao 99.
-Kipa Jussi Jaaskelainen, ikiwa atacheza, hii itakuwa Mechi yake ya 500 ya Ligi huko England.
-Meneja Sam Allardyce atakuwa akisimamia Mechi yake ya 350 ya Ligi.
Tottenham
-Spurs hawajafungwa katika Mechi zao 10
za mwisho za Ligi na wamefungwa moja tu katika Mechi 14 walipochapwa 2-1
na Everton hapo Desemba 9.
-Tottenham, pamoja na Manchester United, ndio Klabu pekee hazijafungwa kwenye LIGI kwa Mwaka 2013.
++++++++++++++++++++++
RATIBA
BPL: BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Jumamosi Machi 2
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v West Bromwich Albion
Everton v Reading
Manchester United v Norwich City
Southampton v Queens Park Rangers
Stoke City v West Ham United
Sunderland v Fulham
Swansea City v Newcastle United
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Wigan Athletic v Liverpool
Jumapili Machi 3
[Saa 1 Usiku]
Tottenham Hotspur v Arsenal
Jumatatu Machi 4
[Saa 5 Usiku]
Aston Villa v Manchester City
++++++++++++++++++++++
No comments:
Post a Comment