Jumatano, 19 Septemba 2012 17:50
Kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI leo
Timu mbili za England, Mabingwa watetezi Chelsea na Manchester United,
wataingia dimbani, wote wakiwa nyumbani, kuanza Mechi zao za Makundi
baada ya jana wenzao, Manchester City kucheza na kufungwa 3-2 na Real
Madrid, na Arsenal kuifunga Montpellier ya Ufaransa bao 2-1.
=====================
RATIBA-UEFA CHAMPIONZ LIGI:
Jumatano Septemba 19
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu]
FC Shakhtar Donetsk v FC Nordsjælland
Chelsea FC v Juventus
LOSC Lille v FC BATE Borisov
FC Bayern München v Valencia CF
FC Barcelona v FC Spartak Moskva
Celtic FC v SL Benfica
Manchester United FC v Galatasaray A.S.
SC Braga v CFR 1907 Cluj
=====================
Leo, Chelsea, wakiwa Stamford Bridge,
wataanza utetezi wa Taji lao kwa kucheza na Mabingwa wa Italy Juventus
ambayo kawaida huwa haishindi Nchini Uingereza kwani katika Mechi zao 11
za mwisho kucheza huko wamefungwa 8 na kutoka sare 3.

Lakini Juventus ya sasa inao Wachezaji wazoefu kama vile Kipa Gianluigi Buffon, Giorgio Chiellini na mchawi Andrea Pirlo.
Katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi,
Serie A, Juve waliipiga Genoa bao 3-1 kwa bao za Emanuele Giaccherini,
Mirko Vucinic na Kwadwo Asamoah.
Nao
Manchester United katika Mechi yao ya nyumbani Old Trafford na
Galatasaray ya Uturuki watakuwa wakiweka rekodi ya kucheza kwa Miaka 18
mfululizo kwenye michuano hii ya Klabu Barani Ulaya.
Pia, upo uwezekano wa Straika wao
mahiri, Wayne Rooney, akacheza sehemu ya Mechi hii baada ya kuanza tena
mazoezi Siku kadhaa zilizopita baada ya kupona jeraha la kuchanwa
pajani.
Mastaa wengine wanaotegemewa kuichezea
Man United kwa mara ya kwanza kwenye michuano hii ni Wachezaji wapya
Robin van Persie na Shinji Kagawa.
Pia, majeruhi wa muda mrefu, Kiungo Darren Fletcher, nae yupo kwenye Kikosi.
Galatasaray wao watawakosa Wachezaji wao wazoefu Mabeki Tomas Ujfalusi na Sabri Sarioglu lakini inao Wachezaji kadh



No comments:
Post a Comment