Jumapili, 02 Septemba 2012 20:21
>>UWANJA wa MTAKATIFU MARIA: Southampton 2 Man United 3Sir Alex Ferguson leo ameweka historia kubwa ya kuwa Meneja wa kwanza kuongoza Klabu katika Mechi 1,000 za Ligi, tena Klabu moja tu, na pia amethibitisha kumnunua Robin van Persie hakufanya makosa baada ya Mchezaji huyo kupiga Hetitriki, licha ya pia kukosa Penati, na kuwapa ushindi Manchester United dhidi ya Southampton, ushindi ambao ni mtamu sana kwao kwa vile walikuwa nyuma kwa Bao 2-1 huku Dakika zimebaki 3 tu.
++++++++++++++++
MAGOLI
Southampton
-Lambert, 16
-Schneiderlin, 55
Man United
-Robin van Persie, 23, 87 na 90
++++++++++++++++
Ule udhaifu wa kihistoria wa Man United wa Difensi yao kuvuja kwa mipira ya juu, ya krosi, leo umethibitika tena baada ya Southampton kupata bao zote zao kwa mipira hiyo.
Southampton ndio waliotangulia kupata bao baada ya Lambert ‘kumpandia’ Rafael na kufunga kwa kichwa lakini Van Persie alisawazisha kufuatia krosi ya Valencia ambayo aliiweka gambani na kumchambua Kipa.
Kipindi cha pili, Southampton wakapiga bao la pili, tena kwa kichwa, pale Evra alipoteleza na kumuacha mfungaji Schneiderlin akipiga kichwa akiwa pekee.
Man United walipata Penati lakini Van Persie akakosa.
Hata hivyo presha ya Dakika za mwisho na umahiri wa umaliziaji wa Robin van Persie ndio uliwapa ushindi Man United.
VIKOSI:
Southampton: Davis; Clyne, Fonte, Hooiveld, Fox; S.Davis Schneiderlin, Ward-Prowse; Puncheon, Lambert, Lallana
Akiba: Rodriguez, Gazzaniga, Lee, Do Prado, Richardson, Mayuke, Seaborne.
Man United: Lindegaard; Rafael, Ferdinand, Vidic, Evra; Carrick, Cleverley, Kagawa; Valencia, van Persie, Welbeck
Akiba: Evans, De Gea, Giggs, Hernandez, Nani, Scholes, Powell.



No comments:
Post a Comment