CAPITAL ONE CUP: Mabingwa Liverpool ugenini na WBA!
Ijumaa, 31 Agosti 2012 08:36
>>MAN United nyumbani na Newcastle, City na Villa, Arsenal v Coventry, Chelsea v Wolves!!Droo ya kupanga Raundi ya Tatu ya CAPITAL ONE CUP, awali lilikuwa likiitwa Carling Cup, imefanyika jana na Mabingwa Watetezi Liverpool wataanza utetezi wao ugenini kwa kucheza na West Bromwich Albion, Timu ambayo sasa inaongozwa na Meneja Steve Clarke aliekuwa Meneja Msaidi Liverpool chini ya Kenny Dalglish kabla wote kufukuzwa, na ambao katika Mechi ya kwanza tu ya Ligi Kuu England waliitwanga Liverpool bao 3-0.
Timu za Manchester United na Manchester City, zote zitaanza nyumbani kwa United kucheza na Newcastle na City kuivaa Aston Villa.
Tottenham wataenda ugenini kucheza na Klabu ya Ligi 1 Carlisle, Everton ugenini na Leeds United na Sunderland ugenini na MK Dons, Timu ya Ligi 1.
Arsenal watakuwa nyumbani kucheza na Coventry City.
Mechi zitachezwa Wiki ya kuanzia Septemba 24.
Crawley will be at home to Swansea and Arsenal host Coventry, while QPR face Reading in an all-Premier League match-up.
DROO KAMILI=RAUNDI ya TATU:
Man United v Newcastle
Man City v Aston Villa
MK Dons v Sunderland
West Brom v Liverpool
Crawley v Swansea
QPR v Reading
Norwich v Doncaster
Bradford v Burton
Preston v Middlesbrough
Arsenal v Coventry
Southampton v Sheffield Wednesday
Chelsea v Wolves
Carlisle v Tottenham
Swindon v Burnley
West Ham v Wigan
Leeds v Everton



No comments:
Post a Comment